Toba (kutoka neno la Kiarabu) ni msimamo wa mtu kujuta dhambi na kwa hiyo kutaka kurekebisha alichoharibu kwa njia hiyo.

Shutuma ya Nabii Nathani dhidi ya Mfalme Daudi na toba ya huyo (Paris Psalter, folio 136v, karne ya 10).

Toba inaweza kujitokeza kwa matendo ya nje ambayo mtu anajipangia ili kubadilika na kufidia. Kati ya matendo hayo, kuna kusali, kusoma vitabu vya dini, kufunga, kujinyima n.k.

Wakristo wanafanya hivyo hasa wakati wa Kwaresima na Juma Kuu. Kwa namna tofauti, Majilio pia ni majira ya toba kwao.

Kwa Waislamu ni hasa mwezi mzima wa Ramadhani.

Katika Biblia Edit

Kadiri ya Biblia, watu wote ni wakosefu na wanapaswa kufanya toba. Kwa sababu hiyo, bila toba hakuna wokovu.

Katika Ukristo Edit

Ungamo la Augsburg linagawa toba pande mbili: "Mmoja ni majuto, yaani hofu inayochoma dhamiri kwa kutambua dhambi; wa pili ni imani ambayo inatokana na Injili au ondoleo, na kusadiki kwamba kwa ajili ya Kristo, dhambi zinasamehewa, na kufariji dhamiri na kuiokoa kutoka hofu."[1]

Katika baadhi ya madhehebu ya Ukristo, kama ya Wakatoliki na ya Waorthodoksi, toba inaweza kukamilishwa na sakramenti maalumu inayoitwa Kitubio au Upatanisho.

Tanbihi Edit

  1. Augsburg Confession, Article XII: Of Repentance. Bookofconcord.org. Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-03-11. Iliwekwa mnamo 2012-09-20.
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.