Billy the Kid ilikuwa jina bandia la Henry McCarty (1859 - 14 Julai 1881) alikuwa mhalifu nchini Marekani wakati wa karne ya 19 aliyekuwa maarufu kwa kuua watu 4-8 kabla ya kuuawa mwenyewe akiwa na umri wa miaka 21 pekee[1].

Billy the Kid.

Masimulizi hutofautiana kuhusu idadi ya watu waliouawa naye hali halisi.[2]

Maisha hariri

Alikuwa mtoto yatima akiwa na umri wa miaka 15. Alikamatwa mara ya kwanza akiwa na miaka 16 kwa sababu aliiba chakula mnamo mwaka 1875. Siku 10 baada ye alipora duka akakamatwa tena lakini alifaulu kukimbia kutoka jimbo la New Mexico kwenda Arizona. Tangu 1877 alijaribu kubadilisha jina akijiita "William H. Bonney" na hapo iko asili ya jina "Billy" (kifupi cha William) jinsi alivyokuwa maarufu.

Mnamo 1877 alimwua mhunzi aliyegombana naye; akarudi New Mexico na akajiunga na kundi la wizi wa ng'ombe. Alishiriki pia katika kundi la wanamgambo walioua watu kwenye fitina ya Kaunti ya Lincoln. Bonney na wanamgambo wenzake wengine wawili baadaye walishtakiwa kwa kuua wanaume watatu.

Umaarufu wake uliongezeka baada ya magazeti mawili kuchapisha habari zake kitaifa kwenye mwaka 1880. Kwenye Desemba 1880 Billy alikamatwa akahukumiwa kunyongwa lakini kwenye Aprili 1881 aliweza kutoroka gerezani akiua wapolisi wawili.

Hatimaye alikutwa na kuuawa na polisi mnamo tarehe 14 Julai 1881.

Katika miaka iliyofuata masimulzi yalitokea kwamba alikuwa hai bado na watu kadhaa walidai eti ndio yeye. Habari zake zilisimuliwa na kupambwa katika vitabu na filamu.

Marejeo hariri

  1. [https://archive.org/details/billykidendlessr00wall Michael Wallis: Billy the Kid - the endless ride], Boston 2007, ISBN 9780393060683 (kupitia archive. org)
  2. "Billy the Kid: How bad was he?".