Bou Regreg
Bouregreg (Kiarabu أبورقراق ou abou rāqrāq) ni mto wa Moroko mwenye urefu wa 240 km. Chanzo chake ni katika milima ya Atlas karibu na mlima wa Jebel Mtourzgane kwenye kimo cha 1627 m juu ya UB. Mdomo uko kati ya mji ya Rabat na Sale. Pande zote mbili za mdomo wa mto palikuwa eneo la Jamhuri ya Bou Regreg iliyojumlisha mjiji ya Rabat na Sale.
Chanzo | Jebel Mtourzgane kwenye Milima ya Atlas |
Mdomo | Atlantiki kwa miji ya Rabat na Sale |
Nchi | Moroko |
Urefu | 240 km |
Kimo cha chanzo | 1627 m |
Mkondo | kawaida 23 m³/s, hadi 1500 m³/s kutegemeana na majira na kiasi cha mvua njiani |
Eneo la beseni | 10,000 km² |
Bouregreg ni kati ya mito mikubwa wa Moroko.