Kambu-ardhi
(Elekezwa kutoka Brachypteracias)
Kambu-ardhi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Kambu-ardhi ni ndege wa familia Brachypteraciidae wanaotokea Madagaska tu. Wanafanana na viogajivu wadogo lakini hawana rangi kali, isipokuwa kichwa cha kambu-ardhi kichwa-buluu na kile cha kambu-ardhi kichwa-chekundu. Hutafuta chakula chini na hula wadudu na watambaachi. Tago lao ni kishimo ardhini. Jike huyataga mayai 1-4.
Spishi
hariri- Atelornis crossleyi, Kambu-ardhi Kichwa-chekundu (Rufous-headed Ground Roller)
- Atelornis pittoides, Kambu-ardhi Kichwa-buluu (Pitta-like Ground Roller)
- Brachypteracias leptosomus, Kambu-ardhi Miraba (Short-legged Ground Roller)
- Geobiastes squamiger, Kambu-ardhi Madoadoa (Scaled Ground Roller)
- Uratelornis chimaera, Kambu-ardhi Mkia-mrefu (Long-tailed Ground Roller)
Picha
hariri-
Kambu-ardhi miraba
-
Kambu-ardhi mkia-mrefu