Kiogajivu
Kiogajivu | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Viogajivu au kambu ni ndege wa tropiki wa jenasi Coracias katika familia Coraciidae. Wanafanana na kunguru wadogo wenye rangi kali: kahawia, buluu na zambarau. Spishi nyingine zina mileli miwili nyingine zina mkia wa mraba. Hula wadudu ambao wanawakamata kutoka kitulio cha juu. Tago lao ni tundu mtini. Jike huyataga mayai 2-4.
Spishi za Afrika
hariri- Coracias abyssinicus, Kiogajivu Habeshi (Abyssinian Roller)
- Coracias caudatus, Kambu Kidari-zambarau (Lilac-breasted Roller)
- Coracias cyanogaster, Kiogajivu Tumbo-buluu (Blue-bellied Roller)
- Coracias garrulus, Kiogajivu wa Ulaya (European Roller)
- Coracias naevius, Kambu Kichwa-marungi (Purple au Rufous-crowned Roller)
- Coracias spatulatus, Kiogajivu Mkia-rungu (Racquet-tailed Roller)
Spishi za mabara mengine
hariri- Coracias benghalensis (Indian Roller)
- Coracias temminckii Purple-winged au Temminck's Roller)
Picha
hariri-
Kambu kidari-zambarau
-
Kiogajivu tumbo-buluu
-
Kiogajivu wa Ulaya
-
Kambu kichwa-marungi
-
Kiogajivu mkia-rungu
-
Indian roller