Njia
Njia ni sehemu au eneo wazi jembamba ambalo hutumiwa na watu, wanyama au magari kupita, lakini pia namna au mbinu ya kufanya kazi au kutatua tatizo fulani.
Mithali maarufu ya Kiswahili inasema, "Penye nia pana njia".
Katika Ukristo
haririYesu alifundisha kufuata njia nyembamba inayopeleka uzimani kuliko ile pana inayofikisha upotevuni (Math 7:13-14).
Zaidi ya hayo, mwenyewe alijitangaza kuwa njia pekee ya kumfikia Baba (Yoh 14:6).
Kadiri ya Matendo ya Mitume, Ukristo uliitwa kwanza "Njia" (22:4).
Tazama pia
haririMakala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |