Bungu
Bungu
Bungu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Lepidoptera (Wadudu walio na mabawa yenye vigamba)
Nusuoda: Glossata
Ngazi za chini

Familia 5:

Bungu ni viwavi wanaotoboa mashina na maganda ya mbegu ya mimea mbalimbali, hususa nafaka na nyasi nyingine. Huitwa funza-mabua pia, lakini jina funza hutumika kwa kawaida kwa viwavi wanaotoboa matunda, k.m. funza-mpamba.

Viwavi wa spishi zote hupenya na kula tishu za ndani ya mashina au maganda ya mbegu ya mimea ya kimelewa, ingawa viwavi wa hatua za kwanza wa kundi la pili wanaweza kuanza kushambulia majicho ya maua, maua na mashina machanga. Wapevu hutofautiana sana kwa kuonekana na wanashiriki tu sifa za jumla za nondo. Tazama makala kuhusu spishi za kibinafsi kwa taarifa zaidi.

Spishi za Afrika

hariri

Crambidae

Gelechiidae

Noctuidae

Pyralidae