Nondo (mdudu)
Kwa maana nyingine za jina hili tazama nondo (maana)
Nondo | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nondo-bundi (Cyligramma latona)
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Nusuoda 5:
|
Nondo ni wadudu wa oda ya Lepidoptera (lepidos = gamba, ptera = mabawa) ambao wanabeba vigamba juu ya mabawa yao. Nondo wanafanana na vipepeo lakini wanatofautiana kwa umbo la vipapasio. Vile vya vipepeo ni kama nyuzi zenye kinundu mwishoni kwao lakini vile vya nondo vina maumbo mbalimbali bila kinundu. Juu ya hiyo takriban nondo wote hukiakia wakati wa usiku na vipepeo hukiakia wakati wa mchana. Kuna zaidi ya spishi 160,000 za nondo.
Utangulizi
haririKama ilivyo kwa vipepeo mzunguko wa maisha wa nondo huwa na hatua nne: yai, kiwavi (lava), bundo na mdumili (imago). Takriban spishi zote huruka wakati wa usiku lakini nyingine huruka jioni na spishi kadhaa wakati wa mchana. Mabawa yakiwa yamefungwa rangi za nondo ni kahawia na/au kijivu hasa na mara nyingi wana rangi za kamafleji. Lakini wakifungua mabawa yale ya nyuma yana rangi kali mara nyingi au mabaka yanayofanana na macho. Hii inashtua mbuai wao kama ndege na mijusi.
Takriban wadumili wote wa nondo hawali, lakina kadhaa hula mbochi. Viwavi vya spishi nyingi vinakula mimea ya mazao. Kwa kawaida wakulima hutumia dawa za kikemikali kuua viwavi hivi. Lakini siku hizi vimekuwa sugu dhidi ya dawa hizi. Kwa hivyo ni bora kutumia dawa za kibiolojia, kama Bt au virusi au kuvu viuawadudu.
Katika sehemu mbalimbali za Afrika viwavi vya spishi kubwa huliwa, k.m. nondo wa mopani katika Afrika Kusini, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Namibia, Zambia na Zimbabwe.
Spishi kadhaa za Afrika
hariri- Cyligramma latona, Nondo-bundi (Cream-striped owl)
- Diparopsis castanea, Funza Mwekundu (Red bollworm)
- Gonimbrasia belina, Nondo wa Mopani (Mopane worm)
- Helicoverpa armigera, Funza-nyanya au funza-matunda (Cotton bollworm)
- Leucania loreyi, Kiwavijeshi bandia (False armyworm)
- Plutella xylostella, Nondo Mdogo wa Kabichi (Diamondback moth)
- Spodoptera exempta, Kiwavijeshi wa Afrika (African armyworm)
- Spodoptera frugiperda, Kiwavijeshi wa Amerika au kiwavijeshi vamizi (Fall armyworm)
- Spodoptera littoralis, Nondo wa Majani ya Mpamba (African cotton leafworm)
- Thaumatotibia leucotreta, Nondo wa Matunda (False codling moth)
Picha
hariri-
Glossata/Noctuidae (Diparopsis castanea - Funza mwekundu)
-
Glossata/Noctuidae (Diparopsis castanea - kiwavi katika tunda la mpamba)
-
Glossata/Noctuidae (Helicoverpa armigera – Funza-nyanya)
-
Glossata/Noctuidae (Spodoptera littoralis – Nondo wa majani ya mpamba)
-
Glossata/Noctuidae (Leucania loreyi - Kiwavijeshi bandia)
-
Glossata/Saturniidae (Gonimbrasia belina - Nondo wa Mopani)
-
Glossata/Plutellidae (Plutella xylostella – Nondo wa kabichi)
-
Glossata/Tortricidae (Thaumatotibia leucotreta – Nondo wa Matunda)
-
Zeugloptera/Micropterigidae (Micropterix tuscaniensis)