Business Line au The Hindu Business Line ni gazeti la kibiashara la Kihindi linalochapishwa na Kasturi & Sons ambao huchapisha ,pia, gazeti la The Hindu. Hili ndilo gazeti jeupe tu katika biashara.

Business Line
Jina la gazeti Business Line au
The Hindu Business Line
Aina ya gazeti *. Gazeti la lugha ya Kiingereza
*. Gazeti la kila siku
Lilianzishwa 1994
Eneo la kuchapishwa Bangalore, Chennai, Coimbatore, Delhi, Hyderabad, Kochi, Kolkata, Madurai
Mangalore, Mumbai, Thiruvananthapuram, Tiruchirapalli, Vijayawada na Visakhapatnam.
Nchi Uhindi
Mhariri *. Bw. N. Ram
*. Bw. K Venugopal
Nakala zinazosambazwa 130,000
Nakala nyingi husambazwa Jumapili
Machapisho husika *. eWORLD
*. Smartbuy
*. BrandLine
*. Life
Tovuti Tovuti Rasmi

Historia

hariri

Business Line lilianza kuchapishwa katika mwaka wa 1994. Huchapishwa kwa mtindo wa gazeti pana na huwa na usambazaji wa nakala takriban 130,000. Nakala za Business Line husambazwa sana katika siku ya Jumapili kulik siku zingine.

Business Line huchapishwa katika maeneo 14:Bangalore, Chennai, Coimbatore, Delhi, Hyderabad, Kochi, Kolkata, Madurai, Mangalore, Mumbai, Thiruvananthapuram, Tiruchirapalli, Vijayawada na Visakhapatnam.

Mhariri mkuu ni Bw. N. Ram na Mhariri Mshiriki ni Bw. K Venugopal. Mwandishi Mohan Padmanabhan huandika makala mengi katika gazeti hili.

Wafanyakazi wake wengi ni waandishi na watafiti. Hili ndilo gazeti pekee lililo na sehemu ya utafiti.

Vipengele

hariri

Jumanne hadi Jumamosi

hariri

Kutoka Jumanne hadi Jumamosi, sehemu kuu ya Business Line ina kurasa 20 - 24. Vichwa vya kurasa ni kama Corporate(Kampuni), Information Technology(Teknolojia ya Mawasiliano), Marketing(Masoko),Editorial & Opinion(Makala ya Mhariri & Maoni) - kurasa mbili, Commodities & AgriBusiness(Bidhaa & Biashara ya Ukulima),Economy(Uchumi), International Business(Biashara ya Kimataifa), Stock Market News(Habari za Soko la Hisa), Stocks & Mutual Fund (kurasa tano), States Variety ,Logistics na Market Watch.

Jumapili

hariri

Jumapili,sehemu kuu ya Business Line ina kurasa 18. Vichwa vya kurasa ni kama Economy(Uchumi),Commodities(Bidhaa),Corporate(Kampuni), International(Kimataifa),Variety, Young Investor(Mwekezaji kijana) na Investment World(Dunia ya Uwezekaji) - kutoka ukurasa wa 8 hadi ukurasa wa 17(mawaidha kuhusu hisa , fedha na amana).

Jumatatu

hariri

Jumatatu,sehemu kuu ya Business Line ina kurasa 16. Vichwa vya kurasa ni kama Market Mood(hali ya Masoko),EconomyUchumi, Information Technology(Teknolojia ya Mawasiliano),AgroBusiness(Biashara ya Ukulima), Transport(Usafiri),'Commodities Investment(Uwekezaji wa Bidhaa), New Manager(Meneja Mpya) - hufahamisha kuhusu viongozi katika dunia ya biashara, Mentor - hufahamisha watu kuhusu kodi, mifumo ya biashara na vitabu, Money & Banking(Pesa na Benki), Editorial & Opinion(Maoni ya Mhariri na Maoni) na States(Majimbo) na Variety.

Machapisho shirika

hariri
Jumatatu eWORLD
Jumatano Smartbuy
Alhamisi BrandLine
Ijumaa Life


Kwenye mtandao wa tarakilishi

hariri

Tovuti ya BUSINESSLINE Online ilianzishwa kwenye mtandao katika mwezi wa Juni 1995. Kurasa za tovuti hii huangaliwa mara milioni 14 kila mwezi duniani kote. Misemo ya Sensex kwenye ukurasa wa kwanza huvutia wengi.

Gazeti hili huuzwa kwa bei ya rupia 4 ($0.10) ya Kihindi katika siku za Jumatatu hadi Jumamosi na bei ya Jumapili ni rupia 3 ($0.075). Magazeti mengine kama The Economic Times na The Financial Express huuza bei sawa katika matoleo yao ya Jumamosi na Jumapili (rupia 7 - rupia 10).Business Line limekuwa na bei sawa wiki nzima isipokuwa Jumapili. Magazeti mengine kama Mint na Business Standard hayachapishwi Jumapili.

Viungo vya nje

hariri