Bwana Myombekere na Mkewe Bugonoka, Mtoto wao Ntulanalwo na Binti Bulihwali

Bwana Myombekere na Mkewe Bugonoka, Mtoto wao Ntulanalwo na Binti Bulihwali ni riwaya iliyo andikwa na mwandishi Mtanzania Aniceti Kitereza. Ni riwaya inayoelezea kwa upana maisha na historia ya Wakerewe katika vizazi vitatu vilivyopita.[1][2]

Ilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1981 katika Kiswahili na Nyumba ya Uchapishaji Tanzania, lakini ilikamilika mwaka 1945 katika lugha mama ya Kikerewe. Kwa kuwa hakuna kampuni ya uchapishaji iliyo kuwa tayari kuchapisha riwaya iyo katika lugha ya kikerewe iliyo hatarini kutoweka, Kitereza alitafsiri mwenyewe riwaya hiyo kwa Kiswahili muda mfupi kabla ya kukutwa na mauti, na ilichukua miaka 35 kupata mchapishaji.

Tangu, imetafsiriwa katika lugha za Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kiswidishi. Riwaya hii ndiyo pekee iliyoandikwa kwa lugha ya Kikerewe, na ni riwaya ya iliyo andikwa kwa kina zaidi kuhusu maisha na desturi za kabla ya ukoloni iliyochapishwa katika lugha ya Kiafrika.[3]

Tafsiri ya Kijerumani ilichapishwa mwaka 1990 katika sehemu mbili ambayo ni wasifu na maelezo baada ya mauti, Ikielezea utamaduni na kiisimu ambao msomaji anaweza kuhitaji.[4] Katika lugha ya kifaransa ili tafsiriwa na Simon Baguma Mweze na Olivier Barlet pia kuchapishwa katika sehemu mbili ilikuwa ni mwaka 1999: Watoto wa mvua[5] na muuaji wa nyoka.[6]Tafsiri ya kiswidi ilifata misingi ya kijerumani lakini ni sehemu ya kwanza pekee iliyochapishwa.

Marejeo

hariri
  1. "Den allra vackraste kärlekshistorien - hd.se". web.archive.org. 2013-09-27. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-09-27. Iliwekwa mnamo 2022-08-09.
  2. "Mkuki Nyanto". mkukinanyota.com. Iliwekwa mnamo 2022-08-09.
  3. "Introduktion till den afrikanska litteraturen". Världslitteratur.se (kwa Kiswidi). 2011-04-29. Iliwekwa mnamo 2022-08-09.
  4. "Aniceti Kitereza: Die Kinder der Regenmacher". www.unionsverlag.com (kwa Kijerumani). Iliwekwa mnamo 2022-08-09.
  5. "LES ENFANTS DU FAISEUR DE PLUIE, Aniceti Kitereza - livre, ebook, epub - idée lecture". www.editions-harmattan.fr (kwa Kifaransa). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-08-09. Iliwekwa mnamo 2022-08-09.
  6. "LE TUEUR DE SERPENTS, Aniceti Kitereza - livre, ebook, epub". www.editions-harmattan.fr (kwa Kifaransa). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-11-10. Iliwekwa mnamo 2022-08-09.