Ugonjwa wa Virusi vya Korona 2019 (kifupi cha Kiingereza: COVID-19) ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Korona 2 (SARS-CoV-2).[3] Dalili zake mara nyingi hujumuisha homa, kikohozi, matatizo ya kupumua, uchovu, maumivu ya kichwa, kutosikia harufu na ladha, maumivu ya koo, kutapika na kuhara. [1] Kuanza kwa kawaida ni siku mbili hadi kumi na nne baada ya kuambukizwa virusi.[1] Baadhi ya watu, hata hivyo, hawapati dalili zozote.[2]

COVID-19
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuMagonjwa ya kuambukiza
DaliliHoma, kikohozi, upungufu wa kupumua, uchovu, kupoteza harufu;[1] baadhi yake hazina dalili[2]
Miaka ya kawaida inapoanzaSiku 2-14 (kawaida 5) kutoka wakati wa maambukizi [1][3]
VisababishiUgonjwa mkali wa kupumua kwa papo hapo coronavirus 2 (SARS-CoV-2)[3]
Njia ya kuitambua hali hiiKipimo cha haraka cha antijeni, kipimo cha PCR[3]
KingaKuweka umbali wa kimwili , barakoa za uso, uingizaji hewa, karantini, chanjo, kuosha mikono[3][4][5]
MatibabuKusaidia tu na kulingana na dalili[6]
DawaWasiolazwa hospitalini: Nirmatrelvir/ritonavir, sotrovimab, molnupiravir[6]
Kali: Tiba ya oksijeni, dexamethasone, remdesivir[6]
Utunzaji za hali ya juu: Tocilizumab, sarilumab[6]
Utabiri wa kutokea kwake20% wanahitaji kulazwa hospitalini[3]
Idadi ya utokeaji wakeKigezo:Matukio ya janga la COVID-19
Vifo~ milioni 20 (kuanzia tarehe 31 Desemba 2021)[7]

Kuenea kwake hutokea hasa wakati mtu aliyeambukizwa anawasiliana kwa karibu na mtu mwingine.[8] Hii inaweza kutokea kwa maambukizi ya hewa au matone madogo yaliyo na virusi.[9][10] Mara chache, virusi hivi vinaweza kuenea kupitia sehemu za juu zilizochafuliwa.[8] Watu wanaweza kusambaza virusi hivi siku mbili kabla ya wao kuonyesha dalili, na kwa ujumla hubakia na sifa ya kuambukiza hadi siku 10, ingawa wale walio katika hali mbaya ua ugonjwa huu wanaweza kuambukiza kwa muda mrefu.[9][11] Utambuzi wake kwa ujumla hufanywa na mmenyuko wa msururua wa kunakili DNA (PCR) au kipimo cha antijeni cha haraka kutoka kwa pua au kuchua usufi wa matone ya kooni. [3]

Hatua za kuzuia ugonjwa huu ni pamoja na kuweka umbali wa kimwili, matumizi ya barakoa ya uso yenye ubora wa juu]], uingizaji hewa wa nafasi za ndani, na kukaa karantini.[3][4][12] Chanjo kadhaa pia hupunguza hatari yake.[5] Mengi ya matibabu yake ni ya kutibu dalili zake na ya kuunga mkono tu.[6] Kwa wale ambao hawahitaji kulazwa hospitalini, lakini wako katika hatari kubwa, nirmatrelvir/ritonavir, sotrovimab, au molnupiravir zinaweza kutumika.[6] Kwa wale wanaohitaji tiba ya oksijeni, wanaweza kutumia dexamethasone na remdesivir.[6] Kwa wale waliohitaji huduma ya hali ya juu tocilizumab au sarilumab zinaweza kuongezwa. [6]

Kati ya watu wanaopata dalili zake, karibu 80% hupona bila kuhitaji kulazwa hospitalini, 15% wanahitaji tiba ya oksijeni, na 5% wanahitaji utunzaji mkubwa.[3] Wazee na wale walio na shida zingine za kiafya wako kwenye hatari kubwa zaidi.[3] Ingawa wengi huimarika baada ya wiki chache, baadhi yao huendelea kuathiriwa na aina mbalimbali za athari (COVID ndefu) kwa miezi kadhaa.[13] Kufikia tarehe 23 Oktoba 2024, angalau matukio 775 yamethibitishwa, ambayo yamesababisha vifo zaidi ya 7,050,000.

Idadi halisi ya vifo ilikuwa; hata hivyo, inakadiriwa kuwa karibu milioni 20 kufikia Desemba 31, 2021.[7] Tukio la kwanza linalojulikana lilitambuliwa huko Wuhan, Uchina, mnamo Desemba 2019. Ugonjwa huu umeenea kote ulimwenguni, na kusababisha janga linaloendelea.

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "Coronavirus Disease 2019 (COVID-19) – Symptoms". Centers for Disease Control and Prevention (kwa American English). 22 Februari 2021. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Januari 2020. Iliwekwa mnamo 19 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 Ma, Q; Liu, J; Liu, Q; Kang, L; Liu, R; Jing, W; Wu, Y; Liu, M (1 Desemba 2021). "Global Percentage of Asymptomatic SARS-CoV-2 Infections Among the Tested Population and Individuals With Confirmed COVID-19 Diagnosis: A Systematic Review and Meta-analysis". JAMA network open. 4 (12): e2137257. doi:10.1001/jamanetworkopen.2021.37257. PMID 34905008.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 "Coronavirus disease (COVID-19)". www.who.int (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 31 Machi 2020. Iliwekwa mnamo 19 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 "Quarantine & Isolation". Centers for Disease Control and Prevention (kwa American English). 9 Januari 2022. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Januari 2022. Iliwekwa mnamo 19 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 "COVID-19 and Your Health". Centers for Disease Control and Prevention (kwa American English). 11 Februari 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 19 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 6.2 6.3 6.4 6.5 6.6 6.7 "Clinical Management Summary". COVID-19 Treatment Guidelines (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Novemba 2021. Iliwekwa mnamo 19 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 7.0 7.1 Wang, Haidong; Paulson, Katherine R; Pease, Spencer A; Watson, Stefanie; Comfort, Haley; Zheng, Peng; Aravkin, Aleksandr Y; Bisignano, Catherine; Barber, Ryan M (Aprili 2022). "Estimating excess mortality due to the COVID-19 pandemic: a systematic analysis of COVID-19-related mortality, 2020–21". The Lancet. 399 (10334): 1513–1536. doi:10.1016/S0140-6736(21)02796-3.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. 8.0 8.1 "COVID-19 and Your Health". Centers for Disease Control and Prevention (kwa American English). 14 Julai 2021. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Aprili 2020. Iliwekwa mnamo 19 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. 9.0 9.1 "Coronavirus disease (COVID-19): How is it transmitted?". World Health Organization (WHO). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Oktoba 2020. Iliwekwa mnamo 6 Desemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Transmission of COVID-19". European Centre for Disease Prevention and Control. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Septemba 2020. Iliwekwa mnamo 6 Desemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Healthcare Workers". Centers for Disease Control and Prevention (kwa American English). 11 Februari 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Juni 2021. Iliwekwa mnamo 19 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "Effectiveness of public health measures in reducing the incidence of covid-19, SARS-CoV-2 transmission, and covid-19 mortality: systematic review and meta-analysis". BMJ (Clinical research ed.). 375: n2997. 3 Desemba 2021. doi:10.1136/bmj.n2997. PMID 34862160.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. "COVID-19 and Your Health". Centers for Disease Control and Prevention (kwa American English). 11 Februari 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Januari 2022. Iliwekwa mnamo 19 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)