Camp Nou
Camp Nou (ambapo hujulikana kama "New stadium" kwa Kiingereza) ni uwanja wa nyumbani wa FC Barcelona. Camp Nou ni uwanja wa mpira uliotengenezwa mwaka 1957.
Camp Nou ina uwezo wa kuchukua watu 99,354, Ni uwanja mkubwa zaidi nchini Hispania na Bara la Ulaya, na ni uwanja wa pili wa soka mkubwa ulimwenguni.
Camp Nou umekuwa ikitumika katika michezo mbalimbali ikiwemo fainali mbili za Kombe la Ulaya / Ligi ya Mabingwa katika mwaka 1989 na 1999, fainali mbili za Kombe la UEFA, michezo ya mwisho ya Kombe la fainali la Inter-Cities, michezo mitano ya mwisho ya UEFA Super Cup, fainali nne za Copa del Rey, michezo ya mwisho ishirini na moja ya Supercopa de España, mechi tano ikiwa ni pamoja na mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia ya 1982 la FIFA.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Camp Nou kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |