Cecil Kellaway
Cecil Kellaway(alizaliwa Agosti 22 1890 - akafariki Februari 28 1973)[1] alikuwa mwigizaji wa Uingereza / Afrika Kusini[2]. Aliteuliwa kuwania tuzo ya Academy Award for Best Supporting Actor kupitia filamu ya The Luck of the Irish na Guess Who's Coming to Dinner 1967.
Cecil Kellaway | |
Amezaliwa | Cecil Kellaway Agosti 22,1890 Afrika Kusini |
---|---|
Amekufa | February 28,1973 |
Nchi | Afrika kusini |
Majina mengine | Cecil Lauriston |
Kazi yake | Muigizaji |
Maisha ya Awali
haririCecil Kellaway alizaliwa Agosti 22 1890 huko Cape Town, Afrika Kusini. Alikuwa mtoto wa wazazi wa Kiingereza, Rebecca Annie (née Brebner) na Edwin John Kellaway, mbunifu na mhandisi. Edwin alihamia Cape Town kusaidia kujenga nyumba za bunge pale Cape Town na alikuwa rafiki mzuri wa Cecil Rhodes, ambaye alikuwa baba wa ubatizo wa Cecil..[3]
Cecil alivutiwa na uigizaji tangu akiwa mdogo.[4] Alisomeshwa katika chuo cha Normal, Cape Town na huko England katika shule ya Grammar. Alisomea uhandisi na aliporudi Afrika Kusini aliajiriwa katika kampuni ya uhandisi. Walakini hamu ya uigizaji ilikuwa kali sana na alikua muigizaji wa wakati wote, akiigiza kwanza katika filamu "Potash na Perlmutter.[3][5][6]
Alitumikia kwa muda mfupi jeshini mnamo 1914 lakini alitolewa nje.[7] Filamu ya mapema aliyoigiza ilijulikana kama The Prince of Pilsen.
Alifanya ziara kwa miaka mitatu kupitia China, Japan, Siam, Borneo, Malaya, Kaskazini na Afrika Kusini na Ulaya, katika filamu kama "Monsieur Beaucaire".
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Cecil Kellaway kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ "Kellaway, Cecil Lauriston (1890–1973)". Kellaway, Cecil (1890–1973). Australian National University. Iliwekwa mnamo 1 Juni 2011.
{{cite book}}
:|work=
ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Obituary, Variety, 7 March 1973, page 78.
- ↑ 3.0 3.1 "GREENROOM GOSSIP", 27 August 1931, p. 16.
- ↑ "THE KELLAWAY FAMILY ON STAGE AND SCREEN", 4 August 1938.
- ↑ "Character Actor Cecil Kellaway is Dead at 79.", 1 March 1973.
- ↑ "The THEATRE & its PEOPLE", 17 July 1924, p. 21.
- ↑ "Round the Shows", 30 July 1925, p. 2.