Nyanda za Juu za Siberia ya Kati
Nyanda za Juu za Siberia ya Kati (kwa Kirusi: Среднесиби́рское плоского́рье, Srednesibirskoye ploskogorye; kwa Kiingereza: Central Siberian Plateau) ni eneo kubwa la milima huko Siberia, mashariki mwa Urusi.
Jiografia
haririNyanda za juu hizo zinafunika sehemu kubwa ya Siberia kati ya mito Yenisei na Lena. Zina eneo la kilomita za mraba 3,500,000. Kwa upande wa kusini zinapakana na milima ya Altai, Salair, Kuznetsk Alatau, Sayan Mashariki na Magharibi, na milima ya Baikal na Transbaikal. Kwa upande wa kaskazini mwa nyanda za juu iko tambarare ya Siberia ya Kaskazini. Upande wa mashariki iko tambarare ya Yakutia na nyanda za Juu za Lena. [1]
Uso wa eneo unaonyesha mabadiliko kati ya sehemu ambazo ni tambarare na safu za milima.[2]
Tabianchi
haririTabianchi ni ya kibara yenye majira ya joto mafupi na majira ya baridi marefu. Sehemu kubwa ya eneo hilo imefunikwa na misitu ya misinobari. Mto mkubwa ni Tunguska ya chini.
Maliasili ya madini ziko nyingi, zikiwa pamoja na makaa ya mawe, madini ya chuma, dhahabu, platini, almasi na gesi asilia.
Marejeo
hariri- ↑ Среднесибирское плоскогорье (Central Siberian Plateau) Ilihifadhiwa 27 Julai 2020 kwenye Wayback Machine. / Great Russian Encyclopedia; in 35 vol.] / Ch. ed. Yu.S. Osipov . - M .: Great Russian Encyclopedia, 2004—2017.
- ↑ "The Central Siberian Plateau". Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 2007-07-13.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nyanda za Juu za Siberia ya Kati kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |