Chacun Pour Soi
"Chacun Pour Soi" ni jina la wimbo uliotoka 24 Juni, 2016 kutungwa na kuimbwa na hayati msanii mkongwe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Papa Wemba akimshirikisha mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Diamond Platnumz. Unatoka katika albamu iliyotolewa baada ya kifo chake - kwa jina la Forever de Génération en Génération. Wimbo umetoka miezi miwili kamili tangu kifo cha Papa Wemba. Papa Wemba alifariki mnamo tarehe 24 Aprili, 2016 jijini Abidjan Ivory Coast. Wimbo ulitayarishwa nchini Ufaransa wakati akifanya ziara ya kumtemblea Fally Ipupa mwishoni mwa mwaka 2015. Wakiwa huko, walikutana na Papa Wemba na kufanya wimbo huu. Tarehe 27 Juni, 2017, mwaka mmoja mbele tangu kutolewa wimbo rasmi, Diamond akatoa vipande vya video akiwa na Papa Wemba wakiwa wanarekodi wimbo huu.[1]
"Chacun Pour Soi" | ||
---|---|---|
Wimbo wa Papa Wemba akiwa na Diamond Platnumz
kutoka katika albamu ya Forever de Génération en Génération | ||
Umetolewa | 24 Juni, 2016 | |
Umerekodiwa | 2016 | |
Aina ya wimbo | Afro-pop, Bongo Flava, Rhumba, Soukous | |
Lugha | Kifaransa Kilingala Kiswahili | |
Urefu | 3:32 | |
Studio | Cantos | |
Mtunzi | Papa Wemba Diamond Platnumz | |
Forever de Génération en Génération orodha ya nyimbo | ||
|
Maudhui
haririWimbo unahusu kuumizana katika mapenzi.
Ubeti wa kwanza
haririBwana anakuwa na subira ya mapenzi, lakini baadaye yanamshinda anaomba poo. Heri abaki peke yake. Papa Wemba anasema (kwa tafsiri isiyo-rasmi);
"Moyo unaniuma, hivi unaskia maumivu na machozi yangu?"
"Niende wapi mbali na haya, nakwenda Dar-Es-Salaam"
"Kilio changu kinazidi cha mutumwa asie kuwa huru"
Halafu anasema; "Kule kule Zanzibar"!
Kisha Chibu anaingia kwa masikitiko makubwa;
Anakumbukia nyakati wako pamoja, asubuhi na mida mingine yenye kutia simanzi. Kwa masikitiko makubwa anaona heri abaki peke yake tu, hakuna namna. Rejea:
"Alfajiri huwa ni kitendawili,
Nafikiri pindi tukiwa wawili,
Tena nakiri inanitesa mwili,
Bora tu niache"
Kiitikio kinasema;
"Chacun pour soi eh, mélodie na nga"
Kwa tafsiri isiyo-rasmi ni;
"Kila mtu kivyake, melody yangu"
"Chacun chez soi eh" "Kila mtu kwake"
Ubeti wa Diamond (wa pili)
haririChibu anaendeleza kilio, masononeko ni makubwa mno. Kuachwa au kutendwa kugumu. Maumivu ya mapenzi jeraha lake halisemezeki. Anamshukuru Mungu kwa yote aliyomtendea. Ipo siku maumivu yake yataondoka kwa kumpata atakayemwondolea maumivu ya moyo. Pamoja na mateso yote, anaomba asimtangazie ubaya huko aendeko. Haitoshi anamtakia kila heri katika safari yake huko aendako. Rejea;
"Ukweli roho inanisonona,
Tena moto hadi sijapona,
Ila naamini Mola ataniona,
Nitakuja pata wakuniponya,
Ila tu chonde ma nikuombe,
Usiniseme vibaya,
Tena nakuombea kuongezewa,
Kwa Mola mwaya"