Abidjan ndio mji mkubwa zaidi nchini Cote d'Ivoire pia ni bandari kuu ya nchi kwenye Ghuba ya Guinea ya bahari ya Atlantiki. Abidjan haiko baharini moja kwa moja lakini kwenye wangwa ya Ebrie inayotengwa na bahari kwa kanda nyembamba ya mchanga.

Jiji la Abidjan
Nchi Cote d'Ivoire
Mkoa Lagunes
Wilaya Wilaya
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 4,707,000
Tovuti:  www.district.abidjan.org

Ilikuwa pia mji mkuu rasmi tangu mwaka 1934 hadi 1983. Kwa sasa imetambulika rasmi kama mji mkuu kiuchumi na bado ofisi nyingi za serikali na balozi za nchi nyingine ziko Abidjan.

Abidjan imekua haraka kuanzia wakazi 65,000 mwaka 1950 hadi 4,707,000 mwaka 2014.[1]

Kuna viwanda vya ngozi, nguo, vyakula na mafuta.

Usafiri jijini Abidjan.
Eneo la Plateau na wangwa wakati wa usiku.

Historia

hariri

Abidjan ilikuwa kijiji tu hadi mwaka 1904. Wakati ule iliteuliwa kuwa mwanzo wa reli ya kuelekea bara. Reli ilianzishwa huko kwa sababu ng'ambo ya wangwa ilikuwepo bandari ndogo ya Port-Bouët. Tangu reli kujengwa Abidjan ilikua haraka. Mwaka 1934 ilitangazwa kuwa mji mkuu wa koloni la Ufaransa la Cote d'Ivoire.

Mwaka 1950 mfereji wa Vridi ulikata kanda la mchanga na kufungua wangwa kwa meli kutoka bahari; wangwa ikawa bandari kubwa yenye usalama mzuri kwa meli, na Abidjan ikawa mji wa bandari iliyosababisha kukua kwa uchumi na kuongezeka kwa watu.

Abidjan kuna chuo kikuu tangu mwaka 1964.

Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka 2002-2007, na hasa 2010-2011 hali ya usalama mjini ilipungua sana.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Abidjan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.