Chai Jing
Chai Jing (Kichina: 柴静; pinyin: Chái Jìng; alizaliwa 1 Januari 1976) ni mwandishi wa habari, mtangazaji wa zamani wa televisheni, mwandishi na mwanaharakati wa mazingira wa China.
Mnamo 1995, Chai alianza kazi yake kama mtangazaji wa redio katika mkoa uitwao Hunan. Kuanzia 2001 hadi 2013, alifanya kazi katika televisheni kuu ya China (CCTV) kama mwandishi wa habari anayeheshimika na mtangazaji. Mnamo 2012 alichapisha wasifu, Utambuzi(Kichina: 看见; pinyin: kànjiàn), ambayo iliuza zaidi ya nakala milioni 1.
Mnamo mwaka 2014, Chai alianza uchunguzi huru kuhusu matatizo yanayokumba mazingira ya China, ambao ulifikia kwa uandishi wa kujifadhiri aliouita Under the Dome (Kichina: 穹顶之下; pinyin: qióng dǐng zhī xià). Kufikia Machi 3, 2015, filamu ilipata maoni zaidi ya milioni 150 nchini China, na hivyo kutoa mwangaza kuhusu mjadala mkubwa kuhusu uchafuzi wa mazingira na sera ya mazingira nchini China. [1] Filamu hiyo ilizuiwa kwenye tovuti za China na mamlaka mnamo Machi 7, 2015. [2] Mwaka 2015 alitajwa kuwa mmoja wa watu 100 mashuhuri zaidi wa jarida la Time.
Marejeo
hariri- ↑ "Phenomenal success for new film that criticises China's environmental policy", The Guardian, March 2, 2015.
- ↑ News Deutsche Welle (German)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chai Jing kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |