Chakonokono
Chakonokono wa kawaida (Duberria lutrix)
Chakonokono wa kawaida (Duberria lutrix)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Lamprophiidae (Nyoka walio na mnasaba na chata)
Fitzinger, 1843
Nusufamilia: Pseudoxyrhophiinae (Nyoka walio na mnasaba na chakonokono)
Dowling, 1975
Jenasi: Duberria
Fitzinger, 1826
Ngazi za chini

Spishi 4:

Chakonokono ni spishi za nyoka za jenasi Duberria katika familia Lamprophiidae. Wamepewa jina hili kwa sababu hula konokono.

Nyoka hawa ni wafupi. Majike yanaweza kufika sm 45 lakini urefu wa wastani ni sm 25 na 35. Kichwa ni kifupi sana na hata mkia ni mfupi wenye ncha kali. Kwa kawaida rangi yao ni kahawia na pengine wana mlia mweusi mbavuni. Kuna wengine weusi kabisa.

Chakonokono hukiakia mchana wakitafuta konokono. Konokono uchi huakiwa tu lakini wale wenye koa huvutwa kutoka koa ile kwanza.

Nyoka hawa hawana sumu na hawaihitaji kwa sababu wanakula konokono tu. Na hawang'ati wakishikwa na watu.

Spishi hariri

Picha hariri

Marejeo hariri

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chakonokono kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.