Chandarua

Chandarua (kutoka neno la Kihindi) ni kitambaa cha wavu kinachotundikwa hasa kitandani ili kumkinga mtu asiumwe na mbu anapolala.

Chandarua kilichoangikwa paani.
Chandarua chenye fremu yake.
Hema lililotengenezwa kwa chandarua.
Chandarua dirishani.

Pia kinaweza kutundikwa katika madirisha na milango ili wadudu wasiingie ndani.

Kwa mbinu hizo binadamu anajaribu kujihami na maradhi yanayosambazwa na mbu na wadudu wengine, kama vile malaria n.k.

Siku hizi wengine wanakitia chandarua dawa ya maji ambayo inaweza kuua wadudu wanapokigusa.