Changes
"Changes" ni wimbo wa hip hop ulioimbwa na kutungwa na hayati Tupac Shakur, awali ulirekodiwa wakati yuko na Interscope ambapo ilirekodiwa na kufanyiwa remixi kati ya 1995 na 1996. Wimbo ulishika nafasi ya #1 nchini Norwei na Uholanzi na kufikia katika ngazi ya kumi bora kwenye nchi kadhaa. Huu ni miongoni mwa nyimbo zake mashuhuri alizotengeneza. Ilitolewa baada ya kifo chake katika albamu ya Greatest Hits, wimbo unazungumzia masuala mbalimbali ambayo yalikuwa yakihusiana na athira ya zama za 2Pac, hasa ubaguzi wa rangi, ukatili wa polisi, madawa ya kulevya, na fujo za kijambazi. Kwa maana nyingine, wimbo umechukua sampuli ya kibao cha mwaka wa 1986 cha "The Way It Is" cha Bruce Hornsby and the Range. Rapa mwenzake E-40 ametumia sampuli hii tayari kwenye wimbo wake, "Things'll Never Change," kwa ajili ya albamu yake ya Tha Hall of Game.
“Changes” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya 2Pac featuring Talent kutoka katika albamu ya Greatest Hits | |||||
Imetolewa | 28 Desemba 1998 | ||||
Muundo | CD | ||||
Imerekodiwa | 1992-1996 | ||||
Aina | hip hop, conscious hip hop, political hip hop | ||||
Urefu | 4:30 | ||||
Studio | Interscope/Amaru/Death Row | ||||
Mtunzi | 2Pac/Bruce Hornsby | ||||
Mwenendo wa single za 2Pac featuring Talent | |||||
|
Chris Hafner-ameongoza muziki wa video ikiwa na mkusanyiko wa vipande kadhaa vya video za awali zilitolewa na 2Pac ikiwa na baadhi ya video za nyumbani na picha zingine ambazo hazijawaji kuoneshwa hapo awali, ipo sawa na muundo wa video ya The Notorious B.I.G. Dead Wrong, ambayo pia ilitolewa mwaka wa 1999.
"Changes" ulipata kuchaguliwa kuwa Wimbo Bora wa Rap kwenye Grammy Awards ya 2000; umebaki kuwa wimbo pekee uliotolewa baada ya msanii kufa na kubaki kwenye kundi hili. Moja kati ya mstari kwenye "Changes" awali ulionekana kwenye toleo la "I Wonder If Heaven Got a Ghetto". Vilevile kuna remixi ya wimbo maarufu uliochanganywa na kibao cha Nelly Furtado, "Say it Right". Lile neno "Huey" ambalo 2Pac analitaja kwenye wimbo ("two shots in the dark, now Huey's dead") ni Huey P. Newton, mwanzilishi wa Black Panther Party. Mnamo mwaka wa 2008, Changes ilipanda hadi Nafasi ya Kwanza kwenye chati za jarida la Billboard Hot Ringtones.
Mnamo mwezi wa Desemba 2009, Vatican wameuweka wimbo wa Tupac Shakur "Changes" kwenye Vatican MySpace Playlist, ambayo ilianzishwa hivi karibuni kwenye UK MySpace mpya. Wimbo huu ni wa kumi miongoni mwa zile za Don Giovanni wa Mozart, na "Uprising" wa Muse bendi.[1]
Michakaliko ya chati
haririChat (1998) | Nafasi |
---|---|
Australian Singles Chart | |
Austrian Singles Chart | |
Belgian Singles Chart | |
French Singles Chart | |
Dutch Singles Chart | |
New Zealand Singles Chart | |
Norwegian Singles Chart | |
Swedish Singles Chart | |
Swiss Singles Chart | |
UK Singles Chart | |
U.S. Billboard Hot 100 | |
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Singles & Tracks | |
U.S. Billboard Hot Rap Singles |
Marejeo
hariri- ↑ "The Vatican's Playlist". MySpace. 10 Desemba 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-01-20. Iliwekwa mnamo 2010-06-15.
- "2 PAC - CHANGES (SONG)". Australian Charts. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-08-09. Iliwekwa mnamo 2009-09-23.