I Wonder If Heaven Got a Ghetto

"I Wonder If Heaven Got a Ghetto" ni single ya kwanza kutolewa baada ya kifo cha 2Pac. Wimbo umeonekana kwenye albamu ya R U Still Down? (Remember Me). Ilitolewa ikiwa upande wa pili kwenye single ya "Keep Ya Head Up".

“I Wonder If Heaven Got a Ghetto”
“I Wonder If Heaven Got a Ghetto” cover
Single ya 2Pac
kutoka katika albamu ya R U Still Down? (Remember Me)
B-side When I Get Free
Imetolewa 1997
Muundo 12" single
Imerekodiwa 1993; 1996
Aina Rap
Urefu 4:40
Studio Interscope
Jive Records
Amaru Entertainment
Mtunzi T. Shakur, D.K. McDowell, Larry Troutman, Lawrence Goodman, Roger Troutman
Mwenendo wa single za 2Pac
"Made Niggaz" "I Wonder If Heaven Got a Ghetto" "Do For Love"

Kuna matoleo mawili ya wimbo huu kwenye albamu ya "R U Still Down? (Remember Me)". Moja ni toleo la remix ya kawaida tu; na lingine ni la "hip-hop remix" toleo ambalo lilirekodiwa wakati yupo Death Row na ilinuiwa kwa ajili ya albamu. Zote mbili tofauti kabisa na toleo halisi ambalo limeingizwa kwenye single ya Keep Ya Head Up.

Jina halisi la wimbo linatokana na mashairi ya Rapa mwenzi wa West Coast Spice 1, ya wimbo wa mwaka wa 1992 "Welcome to the Ghetto."

Baadhi ya sehemu za mashairi ya wimbo huu ulikuja kutumika baadaye kwenye remixi ya single ya "Changes" ambayo ilionekana kwenye albamu ya Vibao Vikali iliyotolewa mnamo mwaka wa 1998.

Rapa Nas amechukua sampuli ya "I Wonder if Heaven's Got A Ghetto" katika wimbo wake wa "Black President" kwenye albamu ya untitled 2008 album. Mstari wa "And though it seems heaven sent/We ain't ready to have a black president" ulitumiwa mara kwa mara ukiwa kama kiitikio.

Muziki wa Video

hariri

Kwenye muziki wa video, taswira ya kwanza ya kamera inaonyesha mtu akielezea mawazo na mitazamo ya Shakur. Baada ya kupigwa risasi, ameanguakia kwenye jumba la Masista lililoitwa Rukahs ('Rukahs' ni 'Shakur' imeandikwa kinyumenyume), huko mjini New Mexico. Leseni ya bamba la gari ambalo Shakur ameingia na mzee linasoma "61671", ambapo inataja tarehe ya kuzaliwa kwa Shakur mnamo 16 Juni 1971. Chumba alichoingia na msichana ni namba 7. Saa iliyokuwa kwa nyuma inaishia 4:03, ni muda rasmi aliokufa Shakur. Mwishoni kabisa, ameenda kwa Amaru Diner, Amaru likiwa jina lake la kati.

Katika sekunde 5 za mwanzo "...rapper tupac shakur shot multiple times" inasikika kutoka katika helikopta.

Video pia inanonesha watu maarufu kadhaa. Mama Teresa anaonekana akiingia kwenye basi, na waliokuwa tayari ndani ya gari ni pamoja na Jimi Hendrix, Martin Luther King Jr., wanachama wa Black Panther Party, na Elvis Presley. Ndani ya baa, Ray Charles anapiga piano, na Snoop Dogg anamsalimia msichana ambaye Tupac alimleta chumbani kwake.