Chanjo ya Kifaduro

Chanjo ya Kifaduro ni chanjo ambayo hulinda dhidi ya kifaduro.[1]

Chanjo ya Kifaduro

Kuna aina mbili kuu: chanjo za chembe-nzima na chanjo isiyo ya chembe.[1] Chanjo ya chembe-nzima hufanya kazi kwa karibu 78% huku chanjo isiyo ya chembe hufanya kazi kwa karibu 71% hadi 85%.[1][2] Ufaafu wa chanjo unaonekana kupungua kwa kati ya 2% na 10% kila mwaka na upungufu wa haraka zaidi kwa chanjo zisizo za chembe. Kutoa chanjo wakati wa ujauzito unaweza kumlinda mtoto.[1] Chanjo hiyo inakadiriwa kwamba imeokoa maisha zaidi ya nusu mwaka wa 2002.[3]

Shirika la Afya Duniani na Kituo cha Udhibiti na Kinga dhidi ya Magonjwa kinapendekeza kwamba watoto wote wapewe chanjo ya kifaduro na ijumuishwe kwenye chanjo za mara kwa mara.[1][4] Hii ni pamoja na watu walio na virusi vya UKIMWI. Vipimo vitatu kuanzia umri wa wiki sita vinapendekezwa kwa watoto wachanga. Vipimo vya ziada vinaweza kutolewa kwa watoto wakubwa na watu wazima. Chanjo hii inapatikana tu kwa mchanganyiko na chanjo nyingine.[1]

Chanjo zisizo za chembe zinatumika sana katika nchi zilizoendelea kwa sababu ya madhara machache. Kati ya 10% na 50% ya watu waliopewa chanjo ya chembe-nzima huwa na wekundu katika sehemu zilizodungwa sindano na homa. Kifafa homa na vipindi virefu vya kulia hutokea kwa chini ya asilimia moja. Kwa chanjo zisizo za chembe, kipindi kifupi cha uvimbe usio hatari kwenye mkono kinaweza kutokea. Madhara kwa aina zote mbili za chanjo, hasa chanjo ya chembe-nzima ni chache kadri mtoto bado ni mchanga. Chanjo za chembe-nzima hazifai kutumika baada ya umri wa miaka sita. Shida hatari za nyurolojia kwa kipindi kirefu hazihusiani na aina yoyote ya chanjo hii.[1]

Chanjo ya kifaduro ilianzishwa mwaka wa 1926.[5] Ipo kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika La Afya Duniani, dawa muhimu zaidi inayohitajika kwenye mfumo wa kimsingi wa afya.[6] Toleo ambalo pia linajumuisha chanjo ya pepopunda, diptheria, polio na Hib hugharimu dola 15.41 kwa kila kipimo mwaka wa 2014.[7]

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Pertussis vaccines: WHO position paper - September 2015" (PDF). Wkly Epidemiol Rec. 90 (35): 433-58. 2014 Aug. PMID 26320265.
  2. Zhang, L; Prietsch, SO; Axelsson, I; Halperin, SA (Sep 17, 2014). "Acellular vaccines for preventing whooping cough in children". The Cochrane Database of Systematic Reviews. 9: CD001478. doi:10.1002/14651858.CD001478.pub6. PMID 25228233.
  3. "Annex 6 whole cell pertussis" (PDF). World Health Organization. Retrieved 5 June 2011.
  4. "Pertussis: Summary of Vaccine Recommendations". Centre for Disease Control and Prevention. Retrieved 12 Dec 2015.
  5. Macera, Caroline (2012). Introduction to Epidemiology: Distribution and Determinants of Disease. Nelson Education. p. 251. ISBN 9781285687148.
  6. "WHO Model List of EssentialMedicines" (PDF). World Health Organization. October 2013. Retrieved 22 April 2014.
  7. "Vaccine, Pentavalent Archived 25 Januari 2020 at the Wayback Machine.". International Drug Price Indicator Guide. Retrieved 8 December 2015.
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chanjo ya Kifaduro kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.