Chatimwamba
Dume wa chatimwamba madole-mafupi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Muscicapoidea (Ndege kama shore)
Familia: Muscicapidae (Ndege walio na mnasaba na shore)
Jenasi: Monticola
Boie, 1822
Spishi: Angalia katiba

Chatimwamba ni ndege wa jenasi Monticola katika familia Muscicapidae. Spishi kadhaa ziliainishwa katika jenasi Pseudocossyphus.

Ndege hawa wana mgongo kahawia, mweusi au buluu, kichwa buluu, buluukijivu au kijivu na tumbo jekundu. Wanatokea Afrika na Asia. Kwa kawaida huonekana juu ya miwamba, majabali na vilima vya mawe. Hula wadudu, watambaachi wadogo na beri. Hujenga tago lao kwa vitu vyororo kama sufu, manyoya na nyuzinyuzi juu ya uoto mfupi, katika ufa wa mwamba au kati ya mawe. Jike huyataga mayai 2-5.

Spishi za Afrika hariri

Spishi ya Asia hariri

Picha hariri