Chevrolet Avalanche

Chevrolet Avalanche ni gari la Kimarekani aina ya pikapu inayo makao ya abiria 5 au 6 lenye milango minne na behewa la kubebea mizigo iliyotengenezwa na kampuni ya magari ya General Motors ya Marekani. Utengenezaji wa avalanche ulianzia Septemba 2001 na kutamatishwa Aprili 2013 ikiwa toleo la pili. Avalanche ilichukua muundo GM wa Chevrolet Suburban na Cadillac Escalade ESV wa kiunzi kirefu kati ya magurundumu.

Chevrolet Avalanche
2007 Chevrolet Avalanche LS
Kampuni ya magariGeneral Motors
ProductionSeptember 2001-April 2013
AssemblySilao, Mexico
ClassFull-size pickup truck
Body style(s)4-door pickup truck\
LayoutFront engine, rear-wheel drive / Four-wheel drive
Wheelbase130.0 in (3,302 mm)
RelatedCadillac Escalade EXT
Chevrolet Suburban
DesignerMarc R. Asposito

Toleo la kwanza 2001–2006Edit

Chevrolet Avalanche
 
ProductionSeptember 2001 - December 2005
PlatformGMT805
Engine(s)
Transmission(s)
Marefu2002–03: 221.7 in (5,631 mm)
2004–06: 221.6 in (5,629 mm)
Upana79.8 in (2,027 mm)
Urefu2002–03: 73.3 in (1,862 mm)
2004–06: 73.6 in (1,869 mm)
RelatedChevrolet Silverado/GMC Sierra
Chevrolet Suburban/GMC Yukon XL
Cadillac Escalade ESV
Cadillac Escalade EXT

Chevrolet Avalanche ilizinduliwa Septemba 2001 kama toleo lilonuiwa kutengenezwa 2002 chini ya GMT800. Mwaka wa kwanza Avalanche iliundwa na plastiki ya kijivu nyeusi kuitofautisha na Suburban/Yukon XL.

Avalanche ya kwanza ilikuwa na aina mbili za injini:

 • injini ya V8 ya Vortec ya lita 5.3 yenye nguvu ya 285 hp (216kW) na uzito wa nusu tani (1500 series)
 • Injini ya V8 ya Vortec ys lita 8.1 yenye nguvu ya 340 hp (253kW) na uzito wa tani robo tatu (2500 series)

Gari hili lilikuwa na mvuto mkubwa kwa uwezo wa kufunguka mlango uliogawa sehemu ya kubebea abiria na behewa la mizigo likiongezea sehemu ya kubebea mizigo. Viti za abiria pia zilikuwa na uwezo wa kufungika kuongeza nafasi kwa dambra. Mwaka wa 2002 Chevrolet Avalanche iliteuliwa kwa tuzo kama SUV bora zaidi Amerika ya Kaskazini na jalida la Motor Trend iliishirikisha kama SUV ya mwaka.[1]

Chevrolet Avalanche Z71 ilikuwa na muundo na uwezo wa kutumika kwa barabara zisizo laini ilhali Z66 ilikuwa na muundo tu bila uwezo ikunuiwa kutumika kwa barabara laini.

Toleo la Pili 2007–2013Edit

Chevrolet Avalanche
 
ProductionApril 2006–April 2013
Model year(s)2007–2013
PlatformGM GMT900 platform (Series GMT940: GMT941)
Engine(s)
Transmission(s)
Marefu221.3 in (5,621 mm)
Upana79.1 in (2,009 mm)
Urefu76.6 in (1,946 mm)
Curb weight5,840 lb (2649 kg)
RelatedCadillac Escalade EXT
Cadillac Escalade ESV
Chevrolet Suburban/GMC Yukon XL
Chevrolet Silverado/GMC Sierra

Toleo ya pili ya Chevrolet Avalanche kwa jina GMT900 Avalanche ilizinduliwa Februari 2006 na utengenezaji rasmi ukaanza Aprili 2006 mjini Silao Mexico.

Sura ya GMT900 hasa mataa ya mbele ilifanana kwa ukaribu na yale ya Tahoe/Yukon na Suburban/Yukan XL. Gari hili pia lilihifadhi viti za abiria za kufunguka na ule mlango unaogawa sehemu ya kubebea abiria na behewa la mizigo sawa na toleo la kwanza.

GMT 900 ilizindua Z71 maalum toleo la pili la Z71 lenye ubora zaidi kwa matumizi kwenye barabara zisizo laini. Injini mpya ya V8 ya Vortec ya lita 5.3 inayotumia diseli oganiki E85. Injini hii mpya ilikuwa na nguvu ya 326hp (243kW), bora kuliko injini ya vortec ya lita 5.3 ya deseli ya hapo awali.

Aina za injini za toloe la pili (toleo la Black Diamond):-

 • V8 VortecMAX ya lita 6.0 (367 horsepower (274 kW) (iliyozinduliwa 2006 - ikasitishwa 2010)

Umaarufu wa Cherolet Avalanche uliendelea na Michael Young mchezaji wa thamani zaidi 2006 wa baseboli alizawadiwa Avalanche ya 2007. Gari hili pia lilitumika kwa sinema mingi za Kimarekani has zenye zinahusishz uharifu kama vile CSI: New York. Kipindi cha ' Speed TV' Bullrun cha mwaka wa 2009 kiliorodhesha Avalanche Z71 nambali ya pili.

Hitimisho la utengenezai wa Chevrolet AvalancheEdit

Aprili 2012, General Motors ilitangaza itaacha utengenezaji wa Avalanche mwaka uliofuata wa 2012 kufuatia kupungua kwa mauzo kwa 2.6% mwaka uliotangulia wa 2011.[2] GM iliendelea na utengenezai wa Cadillac Escalade EXT.

Magari yaliyouzwa MarekaniEdit

Mwaka Magari yaliyouzwa Marekani
2001[3] 52,955
2002[3] 89,372
2003[4] 93,482
2004[4] 80,566
2005[5] 63,186
2006[5] 57,076
2007[6] 55,550
2008[6] 35,003
2009[7] 16,432
2010[8] 20,515
2011[9] 20,088
2012 23,995
2013[10] 16,986

TanbihiEdit

 1. Motor Trend Trucks of the Year Winners List. Motortrend.com (2009-02-24). Iliwekwa mnamo 2018-12-10.
 2. GM announces end of Chevy Avalanche with Black Diamond edition. Autoblog (13 April 2012). Jalada kutoka ya awali juu ya 13 April 2012. Iliwekwa mnamo 2018-12-11.
 3. 3.0 3.1 GM Reports Best December Sales Since 1979. General Motors Media (January 3, 2003). Jalada kutoka ya awali juu ya April 23, 2009. Iliwekwa mnamo 2018-12-10.
 4. 4.0 4.1 GM Reports December 2005 and Year Results. The Auto Channel (January 5, 2006). Iliwekwa mnamo 2018-12-10.
 5. 5.0 5.1 GM Reports 341,327 Deliveries In December. GM Communications (January 3, 2007). Jalada kutoka ya awali juu ya April 23, 2009. Iliwekwa mnamo 2018-12-11.
 6. 6.0 6.1 GM Reports 221,983 Deliveries In December; 2,980,688 Vehicles Sold In 2008. GM Communications (January 5, 2009). Jalada kutoka ya awali juu ya April 23, 2009. Iliwekwa mnamo 2018-12-13.
 7. http://media.gm.com/content/Pages/news/us/en/2010/Jan/0105_Dec_Sales/_jcr_content/iconrow/textfile/file.res/Deliveries%20December%2009.xls
 8. December 2010 Sales: General Motors - Cheers & Gears Forums. Cheersandgears.com. Iliwekwa mnamo 2018-12-12.
 9. http://media.gm.com/media/us/en/gm/news.detail.html/content/Pages/news/us/en/2012/Jan/gmsales.html
 10. http://media.gm.com/dld/content/dam/Media/gmcom/investor/2014/jan/Deliveries-December-2013.pdf

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu: