Mbweta
(Elekezwa kutoka Chlorophoneus)
Mbweta | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mbweta rangi-tatu
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Mbweta ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Chlorophoneus, Malaconotus na Telophorus katika familia Malaconotidae. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara tu. Ndege hawa wana rangi kali kwenye kidari na tumbo, k.m. nyekundu, machungwa, njano au kijani. Mgongo wao ni rangi ya majani au zeituni kwa kawaida. Wana domo nene lenye ncha kwa kulabu. Hula wadudu hasa na vertebrata wadogo pia, mijusi kwa kawaida. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe mtini na jike huyataga mayai 2-4.
Spishi
hariri- Chlorophoneus bocagei, Mbweta Kijanikijivu (Grey-green Bushshrike)
- Chlorophoneus sulfureopectus, Mbweta Kidari-njano Orange-breasted au Sulphur-breasted Bushshrike)
- Chlorophoneus kupeensis, Mbweta wa Mlima Kupe (Mount Kupe Bushshrike)
- Chlorophoneus multicolor, Mbweta Rangi-nyingi (Many-coloured Bushshrike)
- Chlorophoneus nigrifrons, Mbweta Paji-jeusi (Black-fronted Bushshrike)
- Chlorophoneus olivaceus, Mbweta Zeituni (Olive Bushshrike)
- Malaconotus alius, Mbweta wa Uluguru (Uluguru Bush-shrike)
- Malaconotus blanchoti, Mbweta Rangi-tatu (Grey-headed Bush-shrike)
- Malaconotus cruentus, Mbweta Kidari-chekundu (Fiery-breasted Bush-shrike)
- Malaconotus gladiator, Mbweta Kidari-kijani (Green-breasted Bush-shrike)
- Malaconotus lagdeni, Mbweta wa Lagden (Lagden's Bush-shrike)
- Malaconotus monteiri, Mbweta wa Monteiro (Monteiro's Bush-shrike)
- Telophorus cruentus, Mbweta Kidari-pinki (Rosy-patched Bushshrike)
- Telophorus dohertyi, Mbweta Paji-jekundu (Doherty's Bushshrike)
- Telophorus quadricolor, Mbweta Rangi-nne (Four-coloured Bushshrike)
- Telophorus viridis, Mbweta Mrembo (Gorgeous Bushshrike)
- Telophorus zeylonus, Mbweta Kichwa-kijivu (Bokmakierie)
Picha
hariri-
Mbweta kidari-njano
-
Mbweta zeituni
-
Mbweta kidari-pinki
-
Mbweta paji-jekundu
-
Mbweta mrembo
-
Mbweta kichwa-kijivu