Chuo Kikuu cha Mlima Kenya

Chuo Kikuu cha Mlima Kenya ni chuo kikuu ambacho kimeidhinishwa na Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu, kutoa mfumo mzima wa elimu. Ni kimoja kati ya vyuo vikuu vya binafsi nchini Kenya. Kilianzishwa na Profesa Simon Gicharu, ambaye ni mwanaelimu na mjasiriamali.

Aina Chuo Kikuu cha Kibinafsi
Mwanzilishi Profesa Simon Gicharu
Wanafunzi 52,000+ (2015)
Eneo Thika, Kenya
Rangi bluu, rangi ya machungwa, na rangi ya malai
Tovuti www.mku.ac.ke

Kampasi kuu ya Chuo Kikuu cha Mlima Kenya ipo katika mji wa Thika, na kampasi nyingine zipo Nairobi, Parklands, Mombasa, Nakuru, Eldoret, Nkubu, Meru, Kakamega na Kisii. Chuo kikuu cha Mlima Kenya kina vituo vya masomo katika miji ya Malindi, Kisumu, Nyeri na Kericho na ofisi za uuzaji huko Garissa, Isiolo na Kitale.

Dira na dhima

hariri

Misheni ya Chuo Kikuu cha Mlima Kenya ni kutoa elimu ya kiwango cha kimataifa, utafiti na uvumbuzi kwa mabadiliko ya kimataifa na maendeleo endelevu.

Maono yao ni kuwa Kitovu cha Kimataifa cha Ubora katika Elimu, Utafiti na Ubunifu.

Falsafa yao ni kutumia maarifa katika Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya huduma za kibinadamu.

Tunu kuu za Chuo Kikuu cha Mlima Kenya ambayo yanaunda msingi wa ushiriki, ufundishaji na ujifunzaji ni: Ubunifu, Uadilifu, Uhuru wa Kielimu, Usawa, na Ushindani.

 
Mwanzilishi wa Chuo.

Historia

hariri

Mwaka 1996 Dkt. Simon Gicharu alianzisha Taasisi ya Teknolojia ya Thika ambayo ilikuja kuwa chuo kikuu cha Mlima Kenya. Mwaka 2000, Taasisi ilibadilika na kuwa chuo cha kibiashara kinachotoa usimamizi na programu za mafunzo ya kompyuta. Baadaye katika mwaka huo Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia iliitambua taasisi hiyo kuwa taasisi kamili ya elimu ya juu na kuipa kibali kamili cha usajili. Mwaka 2005, Taasisi ya Teknolojia ya Thika ikawa taasisi ya kwanza ya kibinafsi nchini Kenya kutoa mafunzo kwa Wataalamu wa Dawa. Mwaka 2006, Tume ya Elimu ya Juu iliidhinisha ombi la taasisi ya kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta kutoa programu zote za Diploma na Shahada. Mwaka 2011, chuo kikuu cha Mlima Kenya kilitunukiwa idhini na serikali ya Kenya, kwa pendekezo la Tume ya Elimu ya Juu.

Ada na Msaada wa Kifedha

hariri

Chuo Kikuu cha Mlima Kenya kinachukua wanafunzi wanaofadhiliwa na serikali kwa kutumia Kenya Universities and Colleges Central Placement Service (KUCCPS) na pia wanafunzi wanaojifadhili wenyewe. Chuo kikuu pia kinachukua wanafunzi wa kimataifa ambao husafiri kufuata masomo yao nchini Kenya au kujiandikisha kwa elimu-pepe.

 
Moja ya kampasi za chuo kikuu huko Nakuru.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mlima Kenya wanaweza kupata ufadhili kutoka kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Hazina ya Maendeleo ya Maeneobunge, utaalamu, na wafadhili. Chuo kikuu kinaruhusu wanafunzi kulipa ada zao kwa awamu za kila mwezi.

Marejeo

hariri
  • Mount Kenya University Campuses"
  • "Mount Kenya University: Our History"

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Mlima Kenya kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.