Kericho
Kericho ni mji wa Kenya ya kusini magharibi na makao makuu ya kaunti ya Kericho katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki wenye wakazi 42,029 ambao pamoja na vitongoji wa nje hufikia 104,282 kwa eneo kubwa la mji[1].
Kericho | |
Mahali pa mji wa Kericho katika Kenya |
|
Majiranukta: 0°22′0″S 35°18′0″E / 0.36667°S 35.30000°E | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | Kericho |
Idadi ya wakazi (2009) | |
- Wakazi kwa ujumla | 103,911 |
Jiografia
haririKimo cha Kericho kutoka usawa wa bahari ni mita 2,070. Ni kitovu cha eneo la mashamba ya chai. Makampuni makubwa ya chai yana ofisi mjini. Chai inayokuzwa Kericho ni mashuhuru kwa ladha yake nzuri na rangi ya kuvutia. Pia wilaya hii ina wanariadha wa kukimbia mbio za mbali wa hali ya juu sana ambao mara kwa mara wanashinda medali za dhahabu katika mashindano mbalimbali.
Chanzo cha maji cha msitu mau ambacho ni kikubwa kuliko zote nchini Kenya kinapatikana mjini Kericho. Mji huu ni makao makuu ya sekta kubwa ya kilimo cha chai nchini Kenya. Makampuni makubwa ya chai kwa mfano Unilever Kenya' James Finlay na Williamson tea zinapatikana hapa. Chai inayokuzwa hapa huwa inasafirishwa na kuuzwa nchi za Uropa hasa Uingereza. Idadi ya watu wote kwenye kaunti hii ni 752,396 (sensa 2009).
Historia na Utamaduni
haririEneo la mji hukaliwa kiasili ya Wakipsigis ambao ni sehemu ya Wakalenjin. Jamii ya wakipsigis wanasifika kuwa watu walioshika mila zao na pia watu wakarimu. Wanariadha wengi mashuhuri kwa mfano Kipchoge Keino wametoka katika jamii hii.
Chakula mashuhuri cha jamii hii ni kimyet(Ugali) ambayo inaliwa pamoja na mboga za majani, mursik(maziwa ya mgando) na nyama. Chai pia inanywewa sana katika jamii hii, hasa asubuhi na baada ya kula.
Jina la mjii huu linasemekana kwamba linatokana na mganga wa zamani wa Kikipsigis aliyeitwa Kipkerich.
Usafiri
haririUsafiri unaotumiwa sana ni wa magari. Barabara za wilaya hii zipo katika hali nzuri ukilinganisha na wilaya zingine nyingi za nchini Kenya. Barabara kuu tatu zinaelekea mjini Kericho, barabara ya Kisumu-Kericho, barabara ya Kisii-Kericho na barabara ya Nakuru-Kericho. Mabasi na matatu yanatumiwa kwenda miji mingine.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Sensa ya Kenya 2009 Ilihifadhiwa 9 Januari 2019 kwenye Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.
Viungo vya nje
hariri- Population of local authorities - Kericho Ilihifadhiwa 1 Machi 2020 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kericho kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |