Chuo cha upasuaji cha Afrika ya Mashariki, Kati na kusini

Taasisi ya Tiba

The College of Surgeons of East, Central and Southern Afric (kifupi: COSECSA), ni taasisi inayolenga kukuza na kuboresha elimu ya upasuaji kwa matibabu waliohitimu tayari masomo ya tiba katika nchi zote za Afrika Mashariki, ya Kati na Kusini. COSECSA inatoa programu ya mafunzo ya kawaida ya upasuaji na mitihani yenye sifa za kufuzu kimataifa.[1]

COSECSA ni shirika lisilolenga faida ambalo kwa sasa linafanya kazi katika nchi 14 za kusini mwa Jangwa la Sahara: Botswana, Burundi, Kenya, Malawi, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Sudani Kusini, Sudan, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.[1]

Historia

hariri

COSECSA kilianzishwa na Chama cha Wapasuaji wa Afrika Mashariki (Association of Surgeons of East Africa (ASEA). ASEA kilizinduliwa rasmi huko Nairobi, Kenya tarehe 9 Novemba 1950. Mwaka 1996, kutokana na upungufu wa mafunzo ya upasuaji katika eneo hilo, kamati ya ASEA iliamua kuunda Chuo cha Upasuaji cha Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (COSECSA). Azimio hilo lilichukuliwa kutokana na uhaba wa nafasi za masomo ya upasuaji katika vyuo vikuu vilivyopatikana Afrika, pamoja na ugumu wa kujiunga na nafasi kwenye programu za mafunzo ya upasuaji huko Uingereza[2]. Sababu nyingine ilikuwa tofauti baina programu za mafunzo kutoka nchi hadi nchi.

Uzinduzi rasmi wa Chuo hicho ulifanyika Nairobi kwenye Desemba 1999. Mnamo Desemba 2001, katika mkutano mkuu wa kwanza wa mwaka huko Lusaka, baraza la chuo hicho lilichaguliwa pamoja na waanzilishi wake. [3]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 http://bulletin.facs.org/2018/05/cosecsa-collaborates-to-address-surgical-shortages-in-sub-saharan-africa/
  2. http://www.bioline.org.br/pdf?is06100
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-07-26. Iliwekwa mnamo 2021-08-19.
  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo cha upasuaji cha Afrika ya Mashariki, Kati na kusini kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.