Dafu (Siri ya Mtungi)

Dafu ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Patrick Masele. Dafu ni mtu mwenye masihara mengi sana kwa rafiki yake wa karibu, Cheche Mtungi. Historia ya urafiki wao wa karibu haujaoneshwa katika tamthilia, lakini wana urafiki wa karibu kupita kiasi. Tena mara kadhaa Cheche ameonekana kumuendea Dafu kwa kumuomba ushauri wa mambo mengi sana. Sehemu ya kwanza inaanza, Dafu anaonekana kurekebisha kasoro za umeme zilizokuwa zinapatikana katika studio ya Mtungi. Dafu ni mtu mwenye gere sana, halafu hana kipawa cha utongozaji wanawake kama jinsi alivyo Cheche. Mara kadhaa ameonekana kumbembeleza Cheche ampasie japo msichana mmoja. Dafu hakuwahi kutairiwa hadi karibia na sehemu ya mwisho ya msimu wa pili ndipo alipopata suna. Pamoja na kukosa suna tangu zamani, Dafu hana tabia za kimalaya na amekuwa mnasihi mkubwa wa Cheche kuachana na masuala ya wanawake. Ilikuwa Dafu aliyesababisha ndoa ya Cheche na Cheusi Mtungi ikae imara kwa kumsihi sana Cheche aache umalaya wake.[1]

Dafu
muhusika wa Siri ya Mtungi

Taswira ya Dafu (Siri ya Mtungi) (uhusika umechezwa na Patrick Masele)
Imebuniwa na MFDI Tanzania
Imechezwa na Patrick Masele
Idadi ya sehemu 26
Misimu
1, 2
Maelezo
Jinsia Kiume
Kazi yake Fundi wa umeme
Utaifa Mtanzania

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Dafu (Siri ya Mtungi) Ilihifadhiwa 12 Septemba 2016 kwenye Wayback Machine. katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.