Gorée

(Elekezwa kutoka Goree)

Gorée (kwa Kifaransa: Île de Gorée) ni kisiwa cha Atlantiki mbele ya pwani ya Senegal na sehemu ya manisipaa ya Dakar. Ilijulikana kama kituo cha biashara ya watumwa. Hadi kukomeshwa kwa biashara hiyo mwaka 1848 watumwa walipelekwa kisiwani kutoka bara, kufungwa katika jela, kuuzwa kwenye minada na kusombwa hadi Amerika kwa jahazi.

Ramani ya kale ya kisiwa(1772)
Gorée
Gorée inavyoonekana kutoka baharini
Gereza la watumwa

Jiografia

hariri

Kisiwa kina urefu wa m 1000 na upana wa m 300, eneo lake ni ha 36.

Historia

hariri

Kisiwa kiliingia chini ya utawala wa Ureno mwaka 1444 BK. Uholanzi ilivamia Goree mwaka 1588. Katika karne zilizofuata Ufaransa na Uingereza zilishindana juu ya utawala wa kisiwa.

Tangu mwaka 1815 kilikuwa chini ya Ufaransa. Mwaka 1879 idadi ya wakazi ilikuwa 2,956 (Wazungu 50, Machotara 750 na wengine wote Waafrika).

Makumbusho ya Gereza la Watumwa yamekuwa mahali pa utalii. Waamerika weusi walianza kufika kisiwani kutafuta nyayo za mababu waliosombwa kutoka huko wamefungwa kama watumwa.

Mwaka wa 1978, kisiwa cha Goree kiliingizwa na UNESCO katika orodha ya Urithi wa Dunia.

Tazama pia

hariri

Viungo vya Nje

hariri
 
WikiMedia Commons