Ndoo (kundinyota)

(Elekezwa kutoka Dalu (kundinyota))

Ndoo (pia: Dalu) ni kundinyota la zodiaki linalojulikana kimataifa kwa jina lake la kimagharibi la Aquarius[1]. Ni moja ya kundinyota zinazotambuliwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [2]

Ndoo - Dalu (Aquarius) angani
Uchoraji wa msanii wa Karne za Kati unaonyesha jinsi watu walivyoona mbeba maji kati ya nyota za Dalu

Nyota za Ndoo huwa haziko pamoja kihalisi lakini zinaonekana tu vile kutoka duniani. Kwa uhalisi kuna umbali mkubwa kati yao, kama ziko mbali au jirani nasi. Kwa hiyo kundinyota "Ndoo" linaonyesha eneo la angani jinsi tunavyoiona kutoka Duniani.

Jina

Kundinyota hili linajulikana kwa jina la Dalu kwa miaka mingi kwa mabaharia Waswahili walioitumia kutafuta njia baharini wakati wa usiku.[3]

Jina asilia la Dalu linatokana na Kiarabu دلو dalu ambalo linamaanisha "ndoo ya kubebea maji". Jina hili lilipokelewa na Waarabu kutoka kwa Wagiriki wa Kale waliosema Ὑδροχόος hidro-kho-os "mwagiliaji maji" na hao walipokea kundinyota hili kutoka kwa Wababeli.

Katika unajimu wa kisasa katika Afrika ya Mashariki jina "Dalu" limesahauliwa ikiwa kundinyota linaitwa kutokana na ishara yake tu "Ndoo".

Mahali pake

Ndoo iko angani kwenye mstari wa ekliptiki kati ya Mbuzi au Jadi (en:Capricornus) na Hutu (en:Pisces).

Magimba ya angani

Kuna nyota nyingi katika eneo la kundinyota hili lakini zote si angavu sana. Nyota angavu zaidi ni Beta Aquarii ambayo ni nyota jitu kubwa njano yenye mwangaza unaoonekana wa 2.9.

Nyota kadhaa zilitambuliwa kuwa na mifumo ya sayari kwa mfano nyota Gliese 876[4] .

Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miakanuru)
Aina ya spektra
β 22 Sadalsuud 2,90 -3,5 610 G0 Ib
α 34 Sadalmelik 2,95 -3,9 760 G2 Ib
δ 76 Skat 3,27 -0,2 160 A3 V
γ 48 Sadachbia 3,86 0,44 158 A0
λ 73 3,73 -1,7 390 M2 III
ε 2 Albali 3,78 -0,46 230 A1 V
η 62 4,04 0,29 184 B9 IV
θ 43 Ancha 4,17 0,33 191

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Aquarius" katika lugha ya Kilatini ni "Aquarii" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Aquarii, nk.
  2. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  3. ling. Knappert 1993
  4. Astronomy Picture of the Day Gliese 876 has a planet at least 1.6 times as massive as Jupiter, tovuti ya NASA, June 26, 1998

Marejeo

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 45 ff (online kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: THE SWAHILI NAMES OF STARS, PLANETS AND CONSTELLATIONS; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331

Viungo vya Nje


  Makundinyota ya Zodiaki
Majina ya kisasa yanafuatwa kwa mabano na jina la mabaharia na jina la Kilatini (la kimataifa)
 

Kaa (Saratani – Cancer  )Kondoo (Hamali – Aries  )Mapacha (Jauza – Gemini  )Mashuke (Nadhifa – Virgo  )Mbuzi (Jadi – Capricornus  )MizaniLibra  )Mshale (Kausi – Sagittarius  )Ndoo (Dalu – Aquarius  )Nge (Akarabu – Scorpius  )Ng'ombe (Tauri – Taurus  )Samaki (Hutu – Pisces  )Simba (Asadi – Leo  )