Dan Chupong
Chupong Changprung (amezaliwa tar. 23 Machi 1981 mjini Kalasin, Thailand,[1] Kithai: ชูพงษ์ ช่างปรุง, jina la utani la Kithai: "Deaw") ni mwigizaji filamu za martial arts kutoka nchini Thailand. Pia anajulikana kwa jina lake alililopewa na watu Magharibi kama Dan Chupong (jina alilopewa linaandikwa mara mbili tofauti, huandikwa Choopong au Choupong, na jina la kwanza pia huitwa Danny).
Dan Chupong | |
---|---|
Amezaliwa | Chupong Changprung 23 Machi 1981 Mkoa wa Kalasin, Thailand |
Miaka ya kazi | 2003 - Hadi leo |
Alianza akiwa kama mmoja kati ya mwanakundi wa mtalaamu wa stant za kimartial-arts na mkoreografia Panna Rittikrai. Alianza kucheza kwa mara yake ya kwanza katika filamu ya "Bodyguard 4" kwenye Ong-Bak: Muay Thai Warrior. Halafu baadaye akapata kucheza kama muhusika mkuu mnamo mwaka 2004, Born to Fight na filamu ya mwaka wa 2006, Dynamite Warrior. Pia ameonekana katika filamu ya mtaalam Nonzee Nimibutr - Queen of Langkasuka (2008), Somtum (2008) na Ong Bak 2 (hakupata sehemu kubwa).
Kwa kujianda kwa ajili ya shughuli zake za kifilamu, basi Chupong huwa na taratibu za kawaida ya kukimbia na kufanya mazoezi ya viungo. Alichukua masomo ya uigizaji kwa ajili ya uhusika wa filamu ya Dynamite Warrior.[1]
Marejeo
haririViungo vya Nje
haririMakala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dan Chupong kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |