Dynamite Warrior
Dynamite Warrior (Kithai: ฅนไฟบิน au Khon Fai Bin) ni filamu ya Kithailand ya kimartial arts ya mwaka wa 2006. Filamu imeongozwa na Chalerm Wongpim na nyota wa filamu hii ni Dan Chupong (kutoka katika filamu ya Born to Fight).
Dynamite Warrior ฅนไฟบิน (Khon Fai Bin) | |
---|---|
Imeongozwa na | Chalerm Wongpim |
Imetayarishwa na | Prachya Pinkaew |
Nyota | Dan Chupong Panna Rittikrai |
Imesambazwa na | Sahamongkol Film International Magnolia Pictures |
Imetolewa tar. | Thailanda 21 Desemba 2006 Marekani 28 Juni 2007 |
Nchi | Thailand |
Lugha | Kithai |
Hadithi
haririHadithi ipo kwenye seti ya miaka ya 1890 ya Siam.[1] Siang (Dan Chupong) ni bwana shujaa wa Muay Thai na mtaalamu wa rocket ambaye anarudisha nyati maji walioibiwa kutoka kwa wakulima maskini wa Isan na waiba ng'ombe wa kimabavu. Anamtafuta mtu mwenye alama ya tatoo ambaye ndiye aliyeua wazazi wake.
Diwani mmoja wa serikali za mitaa, Lord Waeng (Phutiphong Sriwat), anataka kuunda soko lake la matrekta ya mvuke, hivyo amemkodi pumbavu moja lililofungwa kwa fujo na wizi, "Jizi" (Somdet Kaewleu), kuwaua wafanyabiashara wote wa ng'ombe na kukusanya nyati maji wote na kuwachinja, anachukua wanyama wanawafanyia kazi wakulima ambao wanatumia kwa ajili ya kulimia mchele. Watu wa Lord Waeng wakajikuta wanatia huruma dhidi ya Nai Hoi Sing (Samart Payakaroon), mfanyabiashara wa ng'ombe mwenye nguvu za kichawi za martial arts na tatoo kifuani kwake. Tatoo zile zikamfanya Siang kuwa tayari, na wakati Jizi linajaribu kuiba mifugo ya Sing, Siang ghafla akamvamia Sing, lakini alishindwa.
Baada ya jaribio lile la kuiba ng'ombe wa Sing kushindwa, Waeng akaamua kwenda kumtaka ushauri bwana anayeitwa Mchawi Mweusi (Panna Ritikrai), ambaye awali alilaaniwa na Sing hivyo hawezi kuhimili mwanga wa jua, na hiyo ilikuwa njia pekee ya kuweza kumshinda Sing. Lile Chawi Jeusi likasema: njia pekee ya kurejesha nguvu zake za awali ni kutumia damu ya hedhi ya mwanamke bikra – ambayo ilitolewa kwa binti wake mwenye yule Chawi Jeusi, E'Sao (Kanyaphak Suwankut).
Baada ya kufanikiwa kutengeneza dawa wa kuweza kumwangamiza Sing, kazi ya kupambana naye ilifanywa na Siang mwenyewe kwa sababu yeye alikuwa akiamini kwamba Siang ndiye aliyewaua wazazi wake. Kumbe, haikuwa hivyo - Sing ndiye aliyemwokoa na kumpeleka katika nyumba za ibada ya Mabudha na baadaye kufunzwa namna ya kupambana. Baadaye, Siang anaonekana kwenda kupamba na yule diwani, huku diwani akipata msaada mkubwa kutoka kwa lile Chawi Jeusi.
Shughuli haikuwa ndogo ya kuondoshwa tawala hii, kwani hata yule diwani naye alikuwa keshaanza kujua kutumia nguvu za giza. Mwishowe yule bwana Sing (mfanyabiashara wa ng'ombe) akampa nguvu zake za kichawi bwana mdogo Siang ili aweze kummaliza Chawi Jeusi. Kwa nguvu hizo, alifanikwa kuwangusha wote wawili. Picha inaishia katika jengo jipya la diwani.
Marejeo
hariri- ↑ Lord Waeng mentions that the railway to Korat has been newly opened, placing the time frame of the story sometime in the 1890s. (Historical background Archived 29 Januari 2007 at the Wayback Machine., State Railway of Thailand, 29 Desemba 2006.)
Viungo vya Nje
hariri- Tovuti rasmi ya Dynamite Warrior
ฅนไฟบิน (Khon Fai Bin) - Dynamite Warrior
ฅนไฟบิน (Khon Fai Bin) katika Internet Movie Database - (Kiingereza) Dynamite Warrior
ฅนไฟบิน (Khon Fai Bin) katika Allmovie
Tovuti mbalimbali
hariri- Official website Archived 6 Desemba 2006 at the Wayback Machine. (in Thai and English)
- Trailer (WMV) Archived 30 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
- Khon fai bin katika Internet Movie Database
- (Kiingereza) Dynamite Warrior katika Allmovie
- Dynamite Warrior katika Rotten Tomatoes
- Dynamite Warrior katika Metacritic
- Dynamite Warrior at the Movie Review Query Engine
- Dynamite Warrior katika Sanduku la Ofisi la Mojo
Makala na ripoti
hariri- Review by Peter Nellhaus
- High-kicking cowboys from Isaan Archived 12 Julai 2009 at the Wayback Machine. at The Nation
Picha
hariri- Khon Fai Bin (Dynamite Warrior) Posters Archived 10 Julai 2009 at the Wayback Machine. at Twitch
- Dynamite Warrior sales reel Archived 26 Julai 2009 at the Wayback Machine. at Twitch
- (Thai) Production stills at Deknang Archived 12 Julai 2009 at the Wayback Machine.