Kituo cha umeme cha Dangote Tanzania

 

Kituo cha umeme cha Dangote Industries Tanzania ni kituo cha umeme chenye uwezo wa megawati 45 kinachotumia gesi asilia.[1] Hapo awali, kituo hicho kilipangwa kutoa megawati 75 ikitumia makaa ya mawe. [2]

Mahali

hariri

Kituo cha umeme kipo Mtwara, takriban kilomita 565 kwa barabara upande wa kusini mwa Dar es Salaam. [3] Majiranukta za kituo ni: 10°15'33.0"S, 40°02'27.0"E (Latitudo:-10.259167; Longitude:40.040833).

Muhtasari

hariri

Kituo cha umeme kinamilikiwa na kuendeshwa na Viwanda vya Dangote Tanzania. Kiko karibu na kiwanda cha saruji kinachomilikiwa na kampuni ya Dangote. Kituo cha umeme kinahudumia kiwanda cha saruji pamoja na majengo ya makazi na ya biashara karibu na kiwanda hicho. Kiwanda hiki ni kiwanda kikubwa cha saruji nchini Tanzania kilianza kazi kwenye Desemba 2015.[4]

Kiwanda kina uwezo wa kuzalisha tani milioni 3 za saruji kila mwaka; kwenye miezi Januari hadi Juni 2022 kiliuza tani 944,000 [5]. Dangote Cement kwa jumla ndio watengenezaji wakubwa zaidi wa saruji katika bara la Afrika wenye uwezo wa kuzalisha tani milioni 51.6 kila mwaka.[6] [7] [8]

Kutumia gesi asilia

hariri

Kwenye Agosti 2018 Kampuni ya Dangote ilitia saini mkataba wa miaka 20 na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania kwa ajili ya kununua gesi asilia kwenye kituo hicho kwa madhumuni ya kuzalisha umeme utakaotumika katika utengenezaji wa saruji. Awali gesi ilitolewa ya kuzalisha Kigezo:Invoke:convert ikatarajiwa kuongezwa baadaye hadi Kigezo:Invoke:convert.[9] Kituo kilianza kuzalisha umeme kwa kuchoma gesi asilia tangu MAchi 2021. Gharama za kuzalisha umeme zilishuka kwa asilimia 45 kwenye miezi 15 iliyofuata.[10]

Marejeo

hariri
  1. Alvar Mwakyusa:Tanzania: Hopes for Low Cement Price, allafrica.com ya 21 Agosti 2018
  2. Ng'wanakilala, Fumbuka (4 Novemba 2014). "Dangote Cement Seeks Licence for 75 MW Power Plant In Tanzania". Reuters, United Kingdom. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-06. Iliwekwa mnamo 24 Agosti 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Globefeed.com (24 Agosti 2018). "Distance between Dar es Salaam, Tanzania and Mtwara, Tanzania". Globefeed.com. Iliwekwa mnamo 24 Agosti 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. https://www.dangotecement.com/tanzania/
  5. https://www.cemnet.com/News/story/173174/dangote-cement-s-regional-volumes-fall-by-11-in-1h22.html Dangote Cement's regional volumes fall by 11% in 1H22, tovuti ya cemnet.com ya 03 Agosti 2022
  6. Dangote Cement PLC FULL YEAR 2021 AUDITED RESULTS , [https://dangotecement.com/wp-content/uploads/2022/03/Dangote-Cement-FY-2021-Results-Statement.pdf online hapa (PDF)]
  7. Sotunde, Oluwabusayo (4 Novemba 2014). "Dangote Seeks Approval For Tanzania Power Plant Development". Ventures Africa. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-01-07. Iliwekwa mnamo 24 Agosti 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Staff, Matthew (4 Novemba 2014). "Dangote Cement To Enter 14th African Country With Tanzanian Power Plant". African Business Review (South Africa). Iliwekwa mnamo 24 Agosti 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Mwakyusa, Alvar (21 Agosti 2018). "Tanzania: Hopes for Low Cement Price". Iliwekwa mnamo 24 Agosti 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)Mwakyusa, Alvar (21 August 2018). "Tanzania: Hopes for Low Cement Price". Tanzania Daily News via AllAfrica.com. Dar es Salaam. Retrieved 24 August 2018.
  10. Dangote Cement’s gas transition reduces power costs by 45% in Tanzania, tovuti ya Global Cement ya 30 Juni 2022

Viungo vya nje

hariri