Dardaneli
(Elekezwa kutoka Dardanelles)
Dardaneli (Kituruki Çanakkale boğazi) ni mlango wa bahari katika Uturuki. Zamani za Ugiriki ya Kale na Roma ya Kale ulijulikana kwa jina la Hellespont.
Dardaneli iko kati ya rasi ya Gallipoli upande wa Ulaya na Asia bara. Mlango unaunganisha Bahari ya Mediteranea na bahari ya Marmara. Urefu wa mlango ni 65 km mwenye upana kati ya 1.3 hadi 6 km. Jina la Kituruki hutokana na mji wa Canakkale upande wa mwambao wa Asia.
Wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia Uingereza na Ufaransa walijaribu kushambulia Uturuki hapa. Walishindwa na jeshi lililoongozwa na Mustafa Kemal. Mapigano haya yamejuikana kwa jina la "Gallipoli".
Tangu 1936 mkataba wa Montreux umetawala haki za matumizi kwa meli za mataifa yote.