Bahari ya Marmara
Bahari ya Marmara (Kituruki Marmara denizi, Kigiriki: Propontis) ni gimba la maji ya chumvi kati ya Ulaya na Asia ndani ya nchi ya Uturuki. Imezungukwa na nchi kavu pande zote isipokuwa kuna milango miwili miembamba ya kuiunganisha na [Mediteranea] upande wa kusini na Bahari Nyeusi upande wa kaskazini. Milango hii ni Dardaneli upande wa Mediteranea na Bosporus upande wa Bahari Nyeusi.
![](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/7/70/Sea_of_Marmara_map.png/250px-Sea_of_Marmara_map.png)
Urefu wake ni hadi 282 km na upana 80 km. Kina cha maji hufikia mita 1,300 chini ya UB. Eneo lake ni 11,655 km² na 182 km² ni visiwa ndani yake.
Mji mkubwa kando yake ni Istanbul.