Darmstadti

(Elekezwa kutoka Darmstati)


Darmstadti (zamani: ununnilium ilikuwa jina la kwanza) ni elementi sintetiki yenye namba atomia 110 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni 281. Alama yake ni Ds. Jina latokana na mji wa Darmstadt katika Ujerumani ambako ilitengenezwa mara ya kwanza katika maabara ya "Gesellschaft für Schwerionenforschung (GSI)".

Darmstadti (ununnilium)
Ds-TableImage.svg
Jina la Elementi Darmstadti (ununnilium)
Alama Ds
Namba atomia 110
Mfululizo safu Metali ya mpito
Uzani atomia 281
Valensi 2, 8, 18, 32, 32, 17, 1
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Hali maada inaaminiwa ni mango
Mengineyo tamburania, elementi sintetiki

Elementi ya kutengenezwa katika maabaraEdit

Ni elementi sintetiki au tamburania yaani haipatikani kiasili. Sababu yake ni nusumaisha ya isotopi zake ni fupi mno. 269Ds ina nusumaisha ya mikrosekunde 180; isotopi yenye nusumaisha ndefu ya dakika 1.1 ni 281Ds.

Darmstadti ilitambuliwa mara ya kwanza na wanasayansi wa taasisi ya utafiti wa kinyuklia huko Darmstadt. Walifaulu kutengeneza atomi chache tu katika chombo cha nyuklia tar. 9 Novemba 1994 kwa njia ya myeyungano wa ioni za Plumbi na Nikeli.

Mligano uanofuata waonyesha mmenyuko uliotokea. Pb ni alama ya risasi (metali) (plumbi), Ni nikeli na n ni alama ya neutroni inayobaki mwishoni.

 

JinaEdit

Jina la elementi ilikuwa awali "ununnilium" yaani Kilatini kwa moja-moja-sifuri kwa namba yake 110. Hii ilipatikana kinadharia kabla ya kuwa na elementi lakini wataalamu walikadiria kuwepo wake. Baadaye wanasayansi wa Darmstadt walifaulu kutengeneza elementiki sinteiki sita zilizowahi kutabiriwa kinadharia na kwa sababu hii ofisi kuu ya kumataifa ya wanafisikia iliamua kubadilisha jina kuwa Darmstadt kwa heshima ya maabara katika mji huu.

MatumiziEdit

Kama elementi zote za sintetiki haina matumizi bado zatengenezwa tu kwa kusudi la utafiti. Duniani hazipatikani kiasili tena. Kuna uwezekano ya kwamba ziliwahi kupatikana zamani ila tu kutokana na maisha mafupi ya atomi zao zimeshapotea muda mrefu.


Viungo vya NjeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu: