Darwin Núñez

Mchezaji wa mpira Kutoka chini Uruguay

Darwin Gabriel Núñez Ribeiro (alizaliwa 24 Juni 1999[1]) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa kutoka ncini Uruguay ambaye anacheza katika nafasi ya ushambualiaji ligi kuu ya Uingereza kupitia klabu ya mpira ya Liverpool F.C., na pia kucheza katika timu ya taifa ya Uruguay.

Darwin Núñez (2022)
Darwin Núñez mshambuliaji wa timu ya mpira ya Liverpool ya huko Uingereza
Darwin akiichezea timu ya mpira ya Benfica

Núñez alipitia akademia ya vijana ya Peñarol, akapandishwa hadi timu ya kwanza mwaka wa 2017. Mnamo Agosti 2019, alijiunga na klabu ya Almería inayoshiriki ligi ya Segunda División nchini Hispania . Benfica ilimsajili mwaka 2020 kwa uhamisho wa thamani ya €24 milioni, usajili ghali zaidi katika historia ya soka la Ureno.[2].

Katika msimu wake wa pili, alishinda Bola de Prata katika nafasi ya mfungaji bora wa ligi ya Primeira akiwa amefunga mabao 26 katika michezo 28, akitajwa na kuwekwa katika timu bora ya mwaka ya ligi Kuu na kutajwa kuwa mchezaji bora wa ligi ya Primeira kwa mwaka huo. Liverpool ndipo wakamsajili mnamo Juni 2022 kwa uhamisho wa thamani ya €75 milioni[3] (£64 milioni).

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Darwin Núñez kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.