David Attenborough
Sir David Frederick Attenborough (alizaliwa 8 Mei 1926) ni mwanabiolojia, mwanahistoria wa asili, mtangazaji, na mwandishi wa nchini Uingereza. Anajulikana zaidi kwa kuandika na kuwasilisha, mfululizo wa makala tisa wa historia ya asili pamoja na uchunguzi wa kina wa maisha ya wanyama na mimea duniani akishirikiana na Kitengo cha Historia ya Asili cha BBC, .
Attenborough aliwahi kuwa meneja mkuu katika shirila la utangazaji BBC, alipohudumu kama mtawala wa BBC Two na mkurugenzi wa vipindi wa Televisheni ya BBC katika miaka ya 1960 na 1970. Alianza kujulikana kama mtangazaji wa kipindi cha Zoo Quest mnamo mwaka 1954. Umahiri wake kama mwandishi, mtangazaji na msimulizi umedumu ndani ya miongo minane; ukijumuisha vipindi kama Natural World, Wildlife on One, the Planet Earth franchise, The Blue Planet na mwendelezo wake .Attenborough ndiye mtu pekee aliyeshinda tuzo za BAFTA za ubora wa matangazo ya televisheni, kwa matangazo ya televisheni yenye rangi na yasiyo na rangi na kwa ubora wa 3D na 4K. Katika maisha yake yote amekusanya shahada kadhaa za heshima na tuzo, pamoja na Tuzo tatu za Emmy kwa Simulizi Bora.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu David Attenborough kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |