Ubora ni sifa ya kiumbehai au kitu chochote hasa kulingana na wengine au vingine vya aina ileile.

Ubora


Pengine ubora unatakiwa kulingana na kiwango kinachotarajiwa na watumiaji na sheria za nchi. Kwa ajili hiyo kuna taasisi maalumu zinazothibitishwa kuwa unafikia kiwango hicho. Bila uthibitisho huo bidhaa haiwezi kuuzwa.

Ubora (kibiashara)

hariri

Kwenye biashara uhandisi ubora unatafsiriwa kisayansi kama uwezo wa kutokuwa na mapungufu wa kitu. Ubora ni dhahiri, una sifa fulani ya kujitegemea na unaweza kueleweka tofauti na watu tofauti pia. Watumiaji wanaweza kuangalia pia ubora wa vipimo vya bidhaa, na ubora wa kufanana wa bidhaa.

Wafanyakazi wa msaada wanaweza kupima ubora kwa hatua ambayo bidhaa huweza kuaminika na kudumishwa.

Maelezo

hariri

Kuna vipengele vitano vya ubora kibiashara:

  1. Kuzalisha - kutoa kitu.
  2. Uangalizi - kuhakikisha kwamba jambo linafanyika kwa usahihi.
  3. Kudhibiti ubora - kuhakikisha matokeo yana tabirika.
  4. Usimamizi - kuongoza shirika ili kuongeza utendaji kazi kupitia uchambuzi.
  5. Uhakikishaji - kupata uhakika kuwa bidhaa itakuwa ya kuridhisha.

Ubora uliotumia njia hizi uliendelea kwa kuwa na makampuni ya manunuzi ya NASA,viwanda vya jeshi na nyuklia kuanzia miaka ya 1960 na hii ndiyo sababu ya msisitizo wa kuhakikisha ubora.

  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ubora kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.