Desibeli
(Elekezwa kutoka Decibel)
Desibel (kutoka Kiingereza: decibel; kifupi: dB) ni kizio cha upimaji wa nguvu au ukali. Kinalinganisha vipimo viwili kwa kutumia logi.
Matumizi yake ni hasa katika upimaji wa sauti na katika teknolojia ya umeme kwa kutaja kuongezeka au kupungua kwa volteji au sauti.
Kizio cha msingi ni "bel" na desibel ni sehemu yake ya kumi.
Nyongeza ya desibeli 3 inalingana takriban na kuzidisha nguvu mara mbili.
Kizio cha msingi cha bel kilipata jina lake kwa kumbukumbu ya Alexander Graham Bell aliyekuwa mmoja wa wabunifu wa simu.
Mara nyingi, desibeli hutumiwa kutaja ukubwa wa sauti kulingana na jinsi tunavyoisikia.
Decibel si kipimo sanifu cha SI.
Baadhi ya mifano ya sauti ni:
Kiwango cha Sauti | Mifano |
---|---|
171 dB | Karibu na bunduki kubwa ikipiga risasi |
150 dB | Karibu na injini ya ndege |
110-140 dB | Injini ya ndege kwa umbali wa mita 100 |
130-140 dB | Watu wengi huanza kuhisi maumivu |
130 dB | Baragumu (umbali wa nusu mita) |
120 dB | Tarumpeta ya Vuvuzela (kwa umbali wa mita 1), hatari ya uharibifu wa sikio |
80-90 dB | Trafiki kwenye barabara kuu |
60-80 dB | Gari la abiria |
40-60 dB | Mazungumzo ya kawaida |
20-30 dB | Chumba tulivu sana |
10 dB | Jani kung'aa, kupumua kwa utulivu |
0 dB | Sauti ndogo kabisa inayosikika karibu na sikio |
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Desibeli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |