Dhul Hijjah (mwezi)

Dhu- Hijjah (kwa Kiarabu: ذو الحجة) ni mwezi wa kumi na mbili pia mwezi wa mwisho katika kalenda ya Kiislamu.

Waislamu wakiwa katika msikiti mtakatifu wa Makkah wakati wa Hijjah

Katika maisha ya kidini ni mwezi mtakatifu. Ni mwisho wa mwaka wa Kiislamu pia mwezi wa kuhiji kwenda Makka.

Mwezi huo Waislamu wa nchi zote hukutana hasa Makka kwenye Hajj. Matendo makuu ya Hajj hutokea tarehe 8, 9 na 10 za mwezi huo.