Kumi na mbili
Kumi na mbili ni namba inayoandikwa 12 kwa tarakimu za kawaida na XII kwa namba za Kiroma.
Ni namba asilia iliyopo kati ya kumi na moja na kumi na tatu. Kwa Kiswahili cha pwani kuna pia neno "thenashara".
Vigawo vyake vya namba tasa ni: 2 x 2 x 3.
Katika tamaduni za kale kumi na mbili ilikuwa muhimu hasa kutokana na uhusiano wake na kalenda. Kila mwaka wa jua huwa na vipindi 12 vya mwezi na hivyo miezi 12 ilikuwa msingi wa hesabu ya mwaka.
Utamaduni wa nchi mbalimbali, hasa huko Ulaya uliendelea kutumia mfumo duodesimali [1] badala ya mfumo desimali jinsi ilivyo sasa. Maana vitu vya kuhesabiwa vilijumlishwa kwa makundi ya 12: 12, 144 (12x12), 72 (=nusu ya 144).
Lugha za Ulaya zina majina ya pekee kwa namba hadi 12. Majina yanayounganishwa kwa namna ya "kumi na ..." yanaanzia 13. Kwa 12 kuna pia jina "dazeni" (kutoka Kiingereza dozend).
Pia katika nchi nyingi 12 ilihesabiwa kati ya namba za pekee au namba zenye maana. Tazama matumizi katika Biblia: makabila 12 ya Israeli, Mitume 12 wa Yesu.
Matumizi
haririTanbihi
hariri- ↑ duodesimali inamaanisha "kwenye msingi wa 12"
Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kumi na mbili kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |