Dopamini
Dopamini (kwa Kiingereza: dopamine) ni kemikali inayofanya kazi haswa katika mfumo wa neva kuwasilisha jumbe kutoka nyuroni moja hadi nyingine.
Mwili unaizalisha kemikali hiyo, na mfumo wa neva unaitumia na kutuma ujumbe baina ya seli za neva.
Dopamini inafanya kazi kujuvya namna gani tuhisi furaha: hii ni sehemu kubwa sana ya utofauti wa uwezo wa binadamu kufikiria na kupanga, kwa kuwa inasaidia kujitahidi, kuzingatia na kutafuta mambo tuyapendayo.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dopamini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |