Furaha ni mojawapo kati ya maono ya msingi, pamoja na pendo, hamu, chuki, hofu, huzuni na hasira. Furaha inapatikana pale ambapo umepata kile ulichokipenda na ulichokuwa na hamu nacho.

Watoto wakiwa na Furaha

Neno hili tunaweza kutumia katika hali tofautitofauti. Wapo ambao watalitumia kama jina ila wengine ni hali ya kuwa na amani juu ya ufanyaji wa tendo fulani kwa kuwa hauwezi ukafanya kitu kwa furaha bila ya kuridhia mwenyewe au kuwa na amani nacho. Kwa kufanya hivyo unaweza ukafanya vibaya na kuharibu kabisa. Lakini kama umeridhia nacho, unaweza kufanya kitu hicho kwa umakini na kwa usahihi na unaweza kupendezwa nacho mwenyewe. Kwa mantiki hiyo basi tunaona kwamba katika maisha yetu ya kila siku si vyema kumlazimisha mtu mwingine afanye jambo ambalo hayuko tayari nalo kwa sababu anaweza akafanya kinyume kabisa na unavyotaka na kukusababishia matatizo mengine.