Douglas Wakiihuri
Douglas Wakiihuri (alizaliwa Mombasa, 26 Septemba 1963) ni mwanariadha wa mbio ndefu wa zamani wa Kenya, ambaye alishinda medali ya dhahabu katika mbio za marathon kwenye Mashindano ya Dunia mwaka 1987 huko Roma.[1]
Hakuna mwanariadha mwingine wa kiume wa Kenya aliyewahi kushinda mbio za marathon katika Mashindano ya Dunia au Michezo ya Olimpiki hadi mwaka 2007, wakati Luke Kibet alipokuwa bingwa wa dunia. Mwaka uliofuata, Wakiihuri alishinda medali ya fedha katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto mwaka 1988 huko Seoul, akimaliza nyuma ya Gelindo Bordin.
Mwaka 1989 Wakiihuri alishinda mbio za London Marathoni. Mwaka 1990 alishinda New York Marathoni. Wakiihuri alisifika kwa kuvaa glovu nyeupe wakati wa mbio. Sasa anaendesha kituo cha mazoezi ya mwili marathoni na shule ya mafunzo.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Douglas Wakiihuri kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |