Dragon Ball Z
Dragon Ball Z (kwa Kijapani: Z Hepburn Z: Doragon Bōru Zetto; kifupi: DBZ) ni mfululizo wa vipindi vya televisheni vya katuni vya Japani ambavyo vinatayarishwa na Toei Animation.
Ni kipindi maalumu kilichoandaliwa kwa uangalizi wa familia nzima ili kuwa kama kiburudisho kwa familia.
Katuni hii yaeleza kuhusu sayari ijulikunayo kama sayari ya Vegeta iliyokuja kushambuliwa na kiumbe wa ajabu aitwae Frieza. Frieza alitangaza mapigano na sayari nyingi na kwasababu ya nguvu zake alishinda .alipokuja kutangaza vita na sayari ya Vegeta mfalme aliyetawala hiyo sayari kabla ya ujio wa Frieza aliomba uwepo wa amani lakini Frieza alisisitiza vita ndipo familia ya watu wanne Baba aitwae Bardock, Mama aitwae Geena, mtoto wao wa kwanza aitwae Radits na mtoto wao wa mwisho aitwae cacaraot ilipoamua kuwasafirisha wanao katika sehemu ambayo watakuwa salama na sehemu hiyo ni sayari ya dunia na katika harakati hizo walitokea kumpoteza mtoto wao wa kwanza Radits bila yakutambua kuwa njama za Frieza ni kuilipua sayari yao na kuondoka na watoto wachache ili awape mafunzo ya upiganaji na kuwatumia kama walinzi wake watoto hao walikuwa ni mwana mfalme wa sayari hiyo aitwae Vegeta kama jina la sayari aliyo ishi na mfalme aliye kuwa baba yake kwa mategemeo ya kurithishwa madaraka ya ufalme,Nappor ni mtoto wa generali wa sayari yao na Radits aliyekuwa moja wa wanafamila ya bardock.Cacaraot alipofika duniani kupitia chombo cha angani aliokotwa na mzee huko China aliyeitwa Gohan aliyempa cacaraotjina la Goku na kumlea katika kupigana kwa ajili ya haki na amani.katika maisha ya Goku duniani alijifunza kuhusu hadhina maalumm duniani aitwayo Dragon balls hiyo ni mipira saba ya ajabu ambayo huleta joka la ajabu ambapo ikikusanywa joka huyo ana uwazo wa kutimiza ombi lolote unaloomba kwake.
Katika maisha ya Goku duniani amepitia majaribu pamoja na mafunzo mengi kwa makusudi ya kuzipata dragon balls na katika mapito yote haya amepata marafiki kadhaa ambao ni:
1.Klillin
goku amempata rafiki huyu katika kipindi alichotaka kuanza mafunzo na mwalimu wa upiganaji aitwae roshi alikutana na kijana wa lika lake aliye kuwa na madhumuni ya kuja kujifunza upiganaji kama goku.sababu za kijana huyu kumfuata Roshi kwa ajili ya mafunzo ni:kuonewa na wenzake maana sehemu aliyotokea ina sheheni watawa walio na uwezo wa kupigana na licha ya kukaa pamoja na hao watawa hawajawahi kumfundisha chochote juu ya upiganaji na badala yaka wana muonea klillin na kumfanyisha kazi zote za ndani.
2.Bulma: huyu ni rafiki wa kike aliye kutana na goku kipindi alipokuwa katika kijiji alicho ishi na babu yake(Gohan).Binti huyu alistahajabikaa sana baada ya kumuona mtoto mdogo aliye kuwa goku akiishi katika kijiji kile maana hakuna mtu anaye weza kuishi katika kijiji kile kwa kuwa kuna wanyama wakali ndani ya kijiji hicho.baada ya bulma kuunda urafiki na goku walipata kusaidiana vizuri pamoja katika kutafuta dragon balls maana goku ana maarifa ya upiganaji na bulma ana elimu ya sayansi na teknolojia.Bulma alikubali kumsaidia goku kutafuta dragon balls maana alikuwa na madhumuni ya kuzitafuta dragon balls pia lakini hakuwa na uwezo wa kufanya hivyo bila ya msaada wa mtu kama Goku.
3:Vegeta huyu ndiye mwana mfalme wa sayari ya vegeta na alikuwa mmoja wapo kati ya watu waliopona katika maangamizi ya Frieza na kulelewa na Frieza mwenyewe akiwa pamoja na Radits na Nappor baada ya hawa vijana kupewa mafunzo makali ya kupigana kutoka kwa Frieza na kujitengenezea hali ya kuwa na roho ngumu . Walimtumikia Frieza na kutimiza maagizo yake yote ya kulipua sayari yoyote atakayo na hatima ilifika ambapo Frieza aliagiza kulipuliwa kwa dunia na katika kutimiza agizo hilo radits aliamua kuwahi duniani na kuanzisha uharibifu lakini alifanya hivyo bila kusikiliza mipango ya Nappor na Vegeta ya kusubiria muda kidogo kabla ya kuanza mashambulizi.kati,ka ujio wa radits duniani alikuja na kipima nguvu hicho ni kifa kinachokusaidia kupima nguvu ya mtu yeyote.alipofika duniani alitua milimani na kukutana na mmoja wapo kati ya maadui wakubwa wa goku aitwae Picolo na kuendana na kipima nguvu chake alijua ya kuwa ata kuwa na nguvu sana kwa hiyo alijaribu kupigana naye na alipotaka kumu ua kipima nguvu chake kilihisi nguvu nyingine kubwa zaidi ambayo ingeweza kumpa changamoto kwa hiyo alimsamehe Picolo na kuelekea upande wa hiyo nguvu alipofikia upande wa hiyo nguvu alikuwa katika kisiwa kidogo kilichokuwa na nyumba moja aliangalia watu waliokuwepo na aligundua kuwa aliye kuwa akimtafuta alikuwa ni Goku na alimuona katika mazingira ya karibu alipomuona alikua ameshakuwa mkubwa na alikuwa na mtoto aliye muita jina la babu yake Gohan aliamua kumchukua mtoto wake na kumwambia wewe ni mdogo wangu na hauwezi kufanya kitu chochote kwangu.Goku alichukulia maanani matendo aliyo fanya Radits bila ya kujali kama alikuwa kaka yake au la.kwa sababu hiyo goku aliamua kupigana na radits na katika kupigana na radits aliomba msaada kwa picolo bila ya kujali kuwa alikuwa adui yake na katika kupigana kwao Goku alipigwa na kuumizwa sana na muda huo mwana wake Gohan alikuwa ndani ya chombo cha anga cha Radits alipohisi moyoni maumivu anayoyahisi baba yake alipasua chombo kile cha anga na baada ya kutoka nje ya kile chombo alimpiga Radits pigo moja lililomlegeza na licha ya hiyo kulihitajika kafara ya mtu mmoja ili kumuua radits kikamilifu na Goku ndiye mtu aliyejitolea kufanya hivyo. Goku alipokufa alienda kupeleka nafsi yake kwa mwalimu wa upiganaji aliyemfunza mengi ndani ya mwaka mmoja huku duniani katika kifo cha raditsDalisema maneno yake ya mwisho kwa kuwambia kuwa mwaka mmoja ufuatao watakuja marafiki zangu wawili waitwao Vegeta na Nappor watakuja kuiharibu dinia bila huruma na ndivyo ilivyokuwa kama alivyosema Radits na katika ujio wao waliua marafiki kadhaa wa goku na kusababisha uharibifu wa dragon balls lakini mwisho wa yote walizuiliwa na walipozuiliwa Nappor alikufa na Vegeta alipona na kwanda katika sayari iitwayo Namec iliyozawadiwa dragon balls pia .Baada ya kuondoka kwa vageta na kufa kwa Nappor kulikuwa na amani lakini goku bila marafiki zake hakuweza kuishi kwa amani.
Tokeo la picha la dragon ball z
Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dragon Ball Z kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |