East African Railways and Harbours Corporation
Shirika la reli na bandari za Afrika ya Mashariki (ing. East African Railways and Harbours Corporation (EAR&H)) ilikuwa kampuni ya umma iliyosimamia reli na bandari za Kenya, Uganda na Tanganyika na baadaye Tanzania katika miaka kabla na baada ya uhuru wa nchi hizi.
Historia
haririHadi 1948 kulikuwa na mashirika ya pekee kwa Kenya na Uganda upande mmoja na Tanganyika upande mwingine.
Kenya na Uganda zilikuwa pamoja kwa sababu walikuwa na reli ya pamoja yaani njia ya reli iliyojengwa kuanzia mwaka 1896 kutoka Mombasa kwenda hadi Kisumu mwanzoni , baadaye hadi Kampala ilijulikana kwa jina la Reli ya Uganda.
Tanganyika ilikuwa na mfumo tofauti ya reli iliyoanzishwa wakati wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Reli hii iliendelezwa na Waingereza kwa jina la Tanganyika Railways and Port Services.
Maungano ya huduma katika Afrika ya Mashariki
hariri1948 huduma zote mbili ziliunganishwa kuwa EAR&H. Shirika jipya lilisimamia na kutekeleza kazi za reli, bandari za baharini na pia za ndani halafu huduma ya meli na feri kwenye maziwa makubwa yaani Viktoria Nyanza, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.
Shirika jipya liliendelea kupanushwa mtandao wa reli pa pia kuboreshha huduma ya maji kwa kuleta meli mpxya kwenye Ziwa Viktoria.
Kuvunjwa ka shirika
haririMwaka 1977 viongozi wa nchi za Afrika ya Mashariki walishindwa kupatana juu ya siasa wakavunja Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ya kwanza. Kutokana na hii pia EAR&H ilivunjwa. njia za reloi, mabandari na meli ziligawiwa kwa nchi tatu. Shirika jipya za Kenya Railways Corporation, Tanzania Railways Corporation and Uganda Railways Corporation zilianzishwa.