Edith Achilles

Mwanasaikolojia wa Marekani (1892-1989)

'

Edith Frances Mulhall Achilles
Maelezo zaidi Mwanamke mchanga mweupe aliye na nywele nyeusi zilizogawanywa katikati na amevaa rolls kwenye pande za kichwa chake; amevaa vazi jeupe la lace au blauzi yenye shingo ndefu
Amezaliwa1892
Amefariki1989
Kazi yakeMwanasaikolojia

Edith Frances Mulhall Achilles (Agosti 6, 1892Machi 1989) alikuwa mwanasaikolojia wa Kimarekani aliyefanya kazi katika saikolojia ya shule na kliniki. Katika kipindi cha taaluma yake, Achilles alijikita katika maendeleo ya kumbukumbu na utambuzi kwa watoto, na alichunguza mbinu za majaribio za kupima ujuzi huu.

Maisha ya awali na elimu

hariri

Edith Frances Mulhall Achilles alizaliwa Agosti 6, 1892, huko Boston, Massachusetts. Maisha ya awali ya Achilles hayajulikani sana hadi aliponza masomo yake katika Chuo cha Barnard katika Chuo Kikuu cha Columbia. Baada ya kupata shahada yake ya kwanza ya B.S. mnamo 1914,[1] Achilles alipata shahada ya A.M. na Ph.D. katika Chuo Kikuu cha Columbia mnamo 1915 na 1918, mtawalia.[2]

Mnamo 1917, Edith aliolewa na Paul Strong Achilles, mwanafunzi mwenzake katika Chuo Kikuu cha Columbia. Edith na Paul walikuwa na binti mmoja.

Baada ya kupata Ph.D. yake mnamo 1918, Achilles alianza kufundisha katika Chuo Kikuu cha Columbia na kufanya kazi katika nyanja za saikolojia ya shule na kliniki. Mara baada ya Paul kupata Ph.D. yake na kuanza kufanya kazi katika uwanja wa saikolojia pia, kazi yake ilizidi kuonekana zaidi kuliko ya Edith. Edith alifanya kazi kwa miaka kadhaa katika Chuo Kikuu cha Columbia na Shirika la Saikolojia, ambalo Paul alikuwa mkurugenzi wake kutoka 1932 hadi 1946. Edith na Paul walitalikiana katika miaka ya 1930, lakini Edith aliendelea kufanya kazi katika uwanja wa saikolojia. Alishauriana na Chuo Kikuu cha Oxford na alikuwa mdhamini wa chuo chake cha zamani, Barnard College, kwa miaka kadhaa. Kazi ya Edith katika kipindi cha taaluma yake ilijikita kwenye jinsi watoto wanavyokua na kuendeleza kumbukumbu na utambuzi, na mbinu gani zinaweza kutumiwa kama vipimo vya kuaminika vya maendeleo haya.

Kazi zinazo fanyika

hariri

Edith alichapisha karatasi mbili mashuhuri wakati wa taaluma yake. Ya kwanza, iliyochapishwa mnamo 1920, iliitwa( Experimental Studies in Recall and Recognition.)

Karatasi ya pili ilichapishwa mnamo 1935, kwa ushirikiano na (Clairette Papin Armstrong na M.J. Sacks.) Iliitwa (A Report of the Special Committee on Immigration and Naturalization of the Chamber of Commerce of the State of New York Submitting a Study on Reactions of Puerto Rican Children in New York City to Psychological Tests.)[3]

Angalia pia

hariri
  • Developmental psychology
  • Memory development
  • School psychology
  • Clinical psychology
  • Psychological research and Psychological research methods

Marejeo

hariri
  1. https://digitalcollections.barnard.edu/object/yearbook-1914/mortarboard-1914#page/202/mode/2up
  2. Commencement of Columbia College (kwa Kiingereza). The University. 1908.
  3. Armstrong, Clairette Papin (1935). A Report of the Special Committee on Immigration and Naturalization of the Chamber of Commerce of the State of New York Submitting a Study on Reactions of Puerto Rican Children in New York City to Psychological Tests (kwa Kiingereza). Special Committee on Immigration and Naturalization.
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Edith Achilles kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.