Eisha Stephen Atieno Odhiambo

Eisha Stephen Atieno Odhiambo (1945 - 25 Februari 2009) [1] alikuwa msomi Mkenya aliyezaliwa Muhoroni. Eisha anajulikana kwa mchango wake katika kuelewa hatari zilizomo katika siasa za maarifa na sosholojia ya mamlaka. Dkt Odhiambo alikuwa profesa wa historia katika Chuo Kikuu cha Rice nchini Marekani, ambako aliongoza katika utafiti wa tamaduni. Alisoma katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda na Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya.

Odhiambo alistaafu kutoka Chuo Kikuu cha Rice baada ya kupatwa na ugonjwa uliokatiza kazi yake na kumazimisha arudi nyumbani kwa mkewe Ndere, kaunti ya Siaya, Kenya, kabla ya kifo chake 2009 katika Hospitali ya Aga Khan huko Kisumu. [2]

Bibliografia

hariri

Viungo vya Nje

hariri

Marejeo

hariri
  1. OBIT: E. S. Atieno Odhiambo, H-Net
  2. The Standard, 26 February 2009: Celebrated scholar dies in Kisumu
  Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eisha Stephen Atieno Odhiambo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.